Uwanachama
Uwanachama wa Mtandao wa Policy Forum ni wa hiyari na upo wazi kwa shirikika lolote lisilo la kiserikali lililo sajiliwa Tanzania bara na ambalo malengo yake yanaendana na dira, dhima na malengo ya PF kama yanavyojieleza katika Mpango Mkakati wake.
Faida za Uwanachama
Uwanachama wa PF unaweza kufaidisha shirika lako kama ifuatavyo:
Kujengewa Uwezo
Mtandao wa PF hutoa mafunzo yanayohusu mada mbalimbali kwa wanachama wake kulingana na mahitaji ya wanachama. Pia, wanachama huongezewa maarifa kwa kupitia nyenzo kama vile majarida, taarifa na vipeperushi vinavyochambua sera mbalimbali ambavyo husambazwa kwa njia ya vifurushi.
Upatikanaji wa Watunga Sera/ Wafanya Maamuzi
Mtandao wa PF hutoa nafasi kwa wanachama wake kufanya uchechemuzi kwa watunga sera na wafanya maamuzi kwa malengo ya kushawishi uwepo wa uwazi na uwajibikaji katika matumizi ya rasilimali za umma kwenye sekta mbalimbali ambazo wanachama wanafanyia kazi
Kujumuika Kwenye Mitandao
Wanachama wa PF huweza kujiunga na mitandao mbalimbali ya kitaifa, ya watu binafsi na mashirika yenye dhima zinazoendana, hali hii hupelekea kupatikana kwa makundi yanayoshabihiana ambayo huweza kubadilishana taarifa, mawazo na ujuzi. Policy Forum huratibu warsha za kujifunza, midahalo ya kisera ya kila mwisho wa mwezi, ziara za kimataifa za kujifunza na mikutano ya kutafakari ya kikanda ambayo hutoa fursa ya uanzishwaji wa ubia na mashirika mengine yasiyo ya kiserikali.
Kujulikana
Tunatoa taarifa za kazi za wanachama kupitia tovuti yetu, mitandao ya kijamii na kwa washirika wa kimataifa.
Nguvu ya Kufanya Maamuzi
Kila mwaka, wanachama hupitisha mpango kazi na bajeti ya mtandao pamoja na taarifa za kifedha na utekelezaji za mwaka uliopita. Pamoja na hayo, wanachama wana nguvu ya kupiga kura kuchagua wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi. Kupitia vikundi kazi, wanachama wana nguvu ya kuamua kazi ambazo zitapewa kipaumbele kwenye utekelezaji wa mwaka husika. Wanachama ndiyo huongoza katika utekelezaji wa kazi za mwaka huku jukumu la uratibu likifanywa na sekretarieti
Utafutaji Fedha wa Pamoja
Tunajumuika na wanachama kwenye utafutaji wa fedha za kutekeleza kazi zinazoshabihiana. Pia mtandao hutoa taarifa za nafasi mbalimbali za upatikanaji wa fedha za kufanyia kazi kupitia taarifa za kila wiki. Pia, wanachama hupatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kutafuta fedha na mbinu za kushinda nafasi hizo zinapotangazwa.
Nani anaweza kuwa Mwanachama?
Tunakaribisha maombi ya mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo:
- Ni mashirika yasiyo ya kiserikali yenye angalau miaka miwili ya ufanyaji kazi katika uchechemuzi wa kushawishi utawala bora na uwajibikaji wa matumizi ya rasilimali za umma
- Kujitolea kushiriki kwenye kazi za Policy Forum kama zilivyoainishwa kwenye Mpango Mkakati
- Kuendana na dira, dhima na maadili yetu
- Kuheshimu utofauti wa kitamaduni, kupinga aina zote za ubaguzi na kutofungamana na upande wowote (kutohusika au kupendelea mgombeaji wa kisiasa au chama)
Upo tayari kujiunga? Tafadhali tuma maombi kupitia kwenye fomu hapo chini.
Fomu ya maombi
Ramani inayoonesha mikoa waliyopo wanachama wetu ipo hapo chini pamoja na orodha inayotoa taarifa zaidi.