Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum

Mtandao wa Asasi Zisizo za Kiserikali za Wafugaji (PINGO’s Forum) ni mtandao wa uchechemuzi wa mashirika ya wazawa ambayo kwa sasa yapo 53 yanayojihusisha na utetezi wa haki za makundi ya pembezoni ya wafugaji na wawindaji. Mtandao wa PINGO’s ulianzishwa mwaka 1994 na Asasi sita za wafugaji na wawindaji waliokuwa katika jitihada za kufatuta haki za ardhi na maendeleo kwa ujumla.

Mojawapo ya kazi zinazofanywa na mtandao wa PINGO’s ni:

  1. Kufanya uchechemuzi wa kuhakikisha haki za wafugaji na wawindaji zinatambulika na sheria, sera na mipango mikakati
  2. Kukuza na kulinda haki za kijamii, kiuchumi na kisiasa hasa za wanawake na vijana wa jamii ya wafugaji na wawindaji
  3. Kuhakikisha jamii wa wafugaji na wawindaji zinashirikishwa katika michakato ya sera za mabadiliko ya tabia nchi
  4. Kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa taarifa sahihi kwa ajili ya kufanya maamuzi hasa kuhusiana na haki za binadamu, uwezeshwaji wa wanawake na vijana na mabadiliko ya tabia nchi.

-3.3524992043029, 36.651217968427