Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum
Website

ansaf.or.tz

Sisi ni shirika lisilo la kisiasa, lisilo la kiserikali lililosajiliwa chini ya Sheria ya NGO ya Tanzania ya 2002. Tunawajibika kwa wanachama wetu kama ilivyoainishwa katika Katiba yetu na Kanuni zetu za Maadili. Mtazamo wetu juu ya uwazi na usawa hutufanya kuwa mtandao unaopendwa kwenye sekta ya kilimo.

Tunafanya kazi katika maeneo yafuatayo:

Ugawaji wa Rasilimali

Ukuaji wa kisekta na ufadhili wa umma kwenye kilimo vimekuwa vikipungua. Fedha huathiri uzalishaji na tija. ANSAF inafanya kazi ili kuelewa vizuri kipaumbele cha serikali kwenye sekta ya kilimo, kuwaelimisha wakulima wadogowadogo juu ya mwenendo wa uwekezaji na kufanya kazi kutetea bajeti ya utendaji bora na maisha bora.

Lishe

Umaskini na ukosefu wa chakula ni miongoni mwa vyanzo vya ukosefu wa lishe bora. Tanzania ipo miongoni mwa nchi zenye viwango vya juu zaidi vya utapiamlo sugu ulimwenguni. Kutetea lishe bora kunaweza kuleta athari chanya katika kupunguza umaskini.

Vijana

Vijana wana jukumu la kimkakati katika kupunguza umaskini na kuwa mchango kwa uchumi wa kitaifa. ANSAF, tunaamini kuwa vijana wanaojihusisha katika sekta ya kilimo ni muhimu siyo tu kwa usalama wa chakula bali pia kwa kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana.

-6.7709591530139, 39.261871426513