PELUM ni mtandao wa kikanda wa asasi za kiraia zaidi ya 250 katika nchi 12 za Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika zinazofanya kazi katika eneo la usimamizi shirikishi wa matumizi ya ardhi. PELUM inafanya kazi kuboresha maisha ya wakulima wadogo na uendelevu wa jamii za wakulima, kwa kukuza usimamizi wa matumizi ya ardhi. PELUM ipo Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Lesotho, Botswana, Afrika Kusini, Swaziland na Ethiopia. Makao makuu ya PELUM ni Lusaka, Zambia.
PELUM Tanzania
PELUM Tanzania ni mtandao uliosajiliwa kisheria wa Asasi za Kiraia (AZAKI) ambazo zimekusanyika pamoja kuwezesha na kukuza mitandao, ujifunzaji na utetezi katika usimamizi shirikishi wa matumizi ya ardhi. Ilianzishwa mnamo 1995 na mashirika ya wanachama watano, na kwa sasa imekua hadi mashirika 42 yaliyoonea kote nchini Tanzania. PELUM inahudumia zaidi ya wakulima wadogo wadogo wa kiume na wa kike milioni 1.2. Makao makuu ya PELUM Tanzania yako katika Manispaa ya Morogoro.