Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum

Actions for Democracy and Local Governance (ADLG) imekuwa ikitekeleza mradi wa utawala katika wilaya 6 za Mkoa wa Shinyanga (sasa imegawanyika Shinyanga, Simiyu na Geita) tangu 2011. Sehemu ya msingi ya mradi huo imekuwa kuwajengea uwezo wahamasishaji wa jamii 408 kupitia vikao vya mafunzo na ushauri endelevu. 

ADLG ni mwanachama hai wa (ANSAF) na Policy Forum; hizi ndiyo mitandao ya kitaifa ya AZAKI inayofanya kazi zaidi na inayojulikana nchini Tanzania. ADLG ilijiunga na mitandao hii ili kuwa na uchechemuzi wa kiwango cha kitaifa na pia kuunganisha kwa ustadi masuala yaliyoibuliwa katika ngazi ya serikali za mitaa mpaka ngazi ya Kitaifa. ADLG inashirikiana na ANSAF katika mradii wa Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii ambao umeanza kushika kasi katika wilaya za Sengerema na Bariadi. ADLG pia inafanya kazi na Hakielimu katika masuala ya elimu katika wilaya moja kama mradi wa majaribio. 

-2.5156052380959, 32.919004872853