Children in Crossfire ilianzishwa mnamo 1996. Shirika hili hufanya kazi karika kutatua changamoto zinazokabili watoto na vijana hasa walio katika janga la umaskini na ukosefu wa haki na usawa.
Shirika hili linafanya kazi kwa kushirikiana na mashirika nchini Tanzania na Ethiopia kushughulikia mahitaji ya ukuaji wa watoto wadogo ambao maisha yao yamegubikwa na ukosefu wa haki wa umaskini.
Tunaona elimu ya maendeleo kama sehemu muhimu ya kazi zetu ili kuufanya ulimwengu kuwa mahali pazuri..
Children in Crossfire inafanya kazi zifuatazo:
Njia yetu ni kufanya kazi katika mikoa ambapo mahitaji ya watoto wadogo ni makubwa zaidi. Tunafanya kazi katika mikoa ya Mwanza, Morogoro na Dodoma ili kuboresha maisha kwa maelfu ya watoto. Tunakamilisha kazi hii kwa kushirikiana na mashirika mengine katika ngazi ya kitaifa kushawishi sera na kutetea kuongezeka kwa rasilimali za huduma kwa watoto wadogo.