Machapisho Yetu

Kanuni za Utoaji wa Mikopo na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu za Mwaka 2019

Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/2017-2020/21), pamoja na malengo mengine, unakusudia kuweka mazingira wezeshi kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kujiajiri na kushiriki katika shughuli za kiuchumi kama vile kilimo, ufugaji na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.

Miongoni mwa mikakati ya kutimiza lengo hilo iliyoainishwa katika Mpango huo ni utoaji wa mikopo yenye gharama na masharti nafuu kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP II): Ni kwa Jinsi Gani Tutaboresha Utekelezaji Katika Mamlaka ya Serikali za Mtaa?

Mwanzoni mwa mwaka 2016, Serikali ilizindua FYDP II, kwa lengo la kurekebisha mapungufu ya FYDP I na kutoa mpango makini wakati Tanzania inapoanza kuelekea katika maendeleo ya viwanda katika miaka mitano ijayo (2016 – 2021).

Mwongozo wa Upimaji wa Mwaka: Mfumo wa Ruzuku ya Maendeleo ya Serikali za Mitaa (LGDG)

Upimaji wa Mwaka wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa ni zoezi lililoanzishwa na Mfumo wa Ruzuku ya Maendeleo ya Serikali za Mitaa (LGDG) kupima utendaji kazi wa kila Halmashauri kwa kila mwaka ili kuamua kiasi cha fedha cha LGDG ambacho hatimaye kitapelekwa kwenye Halmashauri husika kwa kuzingatia matokeo ya upimaji huo. Soma zaidi

Maelezo ya Ripoti ya Mbeki Kuhusu Uhamishaji Haramu wa Fedha kutoka Barani Afrika

Februari 2015 Jopo la Ngazi ya Juu Kuhusu Uhamishaji Haramu wa Fedha kutoka Barani Afrika, likiongozwa na Mwenyekiti wake Rais Thabo Mbeki, liliwasilisha ripoti yake kwa Tume ya Umoja wa Afrika/Tume ya Umoja wa Kimataifa ya Kiuchumi Barani Afrika (AUC/ECA). Ripoti ilionesha kuwa nchi za Kiafrika hupoteza kwa wastani dola bilioni 50 kwa mwaka kutokana na uhamishaji haramu wa fedha. Shughuli za kibiashara za sekta binafsi ndizo zinazochangia kwa kiwango kikubwa uhamishaji haramu wa fedha (IFFs), zikifuatiliwa na uhalifu uliopangwa, kisha shughuli za sekta ya umma.

Taarifa ya Ufuatiliaji wa Uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Oktoba 25, 2015

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kwa kushirikiana na Policy Forum, ilifuatilia mchakato wa uchaguzi mkuu wa Tanzania wa mwaka 2015 katika mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Mwanza. Lengo kuu la ufuatiliaji huo lilikuwa ni kutathimini uzingatiaji wa misingi ya kidemokraisa, haki za binadamu, na utawala bora kwenye mchakato mzima wa uchaguzi mkuu wa 2015. Kusoma zaidi bofya hapa.

Mjue Diwani (Toleo la Pili)

Ndugu msomaji, tunayo furaha kukuletea kitabu kipya kiitwacho “Mjue Diwani”  ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wetu wa kikundi kazi cha serikali za mitaa wa kuwaelimisha wananchi kuhusu utawala wa Serikali za Mitaa na
kukuza uwajibikaji katika jamii. Kusoma zaidi bofya hapa

Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2015/2016: Toleo la Wananchi (Limetolewa na Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Policy Forum)

Hili ni toleo lingine la  Bajeti Toleo la Wananchi ambalo linaelezea Bajeti ya Serikali kwa mwaka  wa  fedha  2015/16  kwa  lugha rahisi  inayoeleweka  kwa wananchi.

Maswali Yetu Muhimu kwa Serikali ya Tanzania

Mfumo wa Uongozi / utawala wa sasa wa Tanzania utafikia mwisho wake katika miezi michache ijayo. Hii inatoa njia kwa mfumo mpya kuchukua hatamu ikitegemewa kuwa na mikakati mipya au iliyoboreshwa kusukuma maendeleo ya kiuchumi.

Makosa ya Rushwa Katika Chaguzi Tanzania

Policy Forum na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) tunakuletea tena chapisho hili la tatu katika mtiririko wa machapisho yanayohusu elimu kwa umma juu ya kupambana na rushwa.
Mtakumbuka kuwa chapisho letu la kwanza la pamoja lilihusu sheria mpya namba 11 ya mwaka 2007 ya kuzuia na kupambana na rushwa hapa Tanzania,

Chapisho hili linaweka wazi sheria zetu zinavyosema kuhusu makosa yarushwa katika chaguzi hapa nchini Tanzania na adhabu zinazotolewa kwa makosa husika,

Ilani ya Uchaguzi ya Azaki Tanzania (2015)

Wazo la kuweka wazi matakwa ya Asasi za Kiraia (AZAKI) juu ya Tanzania tuitakayo katika mfumo wa ilani ya uchaguzi lilitokana na mkutano wa watetezi wa haki za binadamu. Kusoma zaidi bofya hapa.

Utawala wa Kidemokrasia Katika Jamii (Toleo la 8)

UTANGULIZI
Mwananchi ana wajibu na majukumu yake kuhakikisha kuwa Kiongozi aliyemchagua au kuteuliwa anatimiza wajibu wake ipasavyo katika viwango vinavyokubalika katika eneo la kijiji/mtaa kulingana na mipango na makubaliano ya vikao vya kisheria vya kijiji na mtaa. Kila mwananchi ana wajibu wa kupinga na kukataa kila aina ya uovu katika jamii ikiwemo rushwa, uonevu, wizi, ubadhirifu wa mali za umma na ya watu binafsi.

Mjue Diwani

Kijitabu cha Rasimu ya Katiba na Mwelekeo wa Uhuru na Ufanisi wa Serikali za Mitaa

Kitabu hiki ni mfululizo wa mchango wa Policy Forum kwenye mchakato wa kuandika katiba mpya hapa nchini Tanzania toka uanze mnamo Disemba 2010, kitabu hiki ni cha tatu katika mfululizo huo wa vitabu vilivyotolewa na Policy Forum kuchangia uelewa. Kusoma zaidi bofya hapa.

Tathmini ya Usimamizi wa Rasilimali hupima ubora wa usimamizi katika sekta za mafuta, gesi, na uchimbaji wa madini

Uchimbaji madini huchangia asilimia 5 ya pato ghafi la ndani na theluthi moja ya mauzo ya nje.. Mwaka 2011 thamani ya mauzo ya nje ya madini ilifikia kiasi cha dola za marekani bilioni 2.1, kati ya hizo zaidi ya asilimia 95 zilitoka katika machimbo sita ya dhahabu. Kusoma zaidi bofya hapa

Rasimu ya Pili ya KATIBA Inasemaje? Chapisho la Lugha Nyepesi

Tanzania ipo katika mchakato wa Katiba tangu mwanzoni mwa mwaka 2011. Hatua kadhaa zimeshapitiwa katika mchakato huu muhimu kwa Taifa letu kama ifuatavyo; Kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya
mwaka 2011, kuundwa kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa mujibu wa sheria, Tume kuanza kazi kwa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya, Tume kutoa Rasimu ya kwanza ya Katiba na hatimaye Rasimu ya pili
ya Katiba.

BRICS (Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini):Mkakati Mbadala wa Ushirikiano wa Kimaendeleo?

Mandhari ya hali halisi ya ushirikiano wa kimaendeleo inabadilika huku kukiwa na ongezeko la washirika wapya ambao ni Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini, unaojulikana kwa pamoja kama BRICS . Washirika hawa wapya ambao

Mwongozo wa Utawala Bora

Kijitabu hiki cha Mwongozo wa Utawala Bora ni mfululizo wa utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora pamoja na Policy Forum ya kukuza utawala bora nchini. Vile vile, kijitabu hiki ni mchango wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora pamoja na Policy Forum katika kusaidia juhudi za Serikali za kuimarisha utawala bora katika ngazi zake zote.

Kukisoma bofya hapa

Tathmini wa Usimamizi wa rasilimali kwa Mwaka 2013

Uchimbaji madini huchangia asilimia 5 ya pato ghafi la ndani na theluthi moja ya mauzo ya nje.. Mwaka 2011 thamani ya mauzo ya nje ya madini ilifikia kiasi cha dola za marekani bilioni 2.1, kati ya hizo zaidi ya asilimia 95 zilitoka katika machimbo sita ya dhahabu. Tanzaniapia inazalisha shaba, madini fedha, almasi, na gesi asilia. kusoma soma kiambatanisho hapa chini

Katiba Mpya na Ufanisi wa Serikali za Mitaa Tanzania

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni katiba iliyotungwa
mwaka 1977. Katiba hii inaielezea Tanzania kama nchi ya kidemokrasia,
inayofuata misingi na haki za binadamu na siasa yake ni ya vyama vingi.
Katiba ni sheria mama ya nchi inayowawezesha wananchi kujitambua
kama taifa na ya kiutawala inayoelezea mgawanyo wa madaraka na
majukumu ya vyombo mbalimbali vya dola.
Ibara ya 6 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inatoa maana ya neno
“Serikali” ambayo ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya

HAKI ZA MAZINGIRA, UHIFADHI NA UTUNZAJI MAZINGIRA TANZANIA:UHALALI WA KUINGIZWA KWAKE KATIKA ITAKAYOKUWA KATIBA MPYA

Mada hii inalenga katika kuchochea mjadala na kutoa taarifa zaidi katika mchakato unaoendelea wa kupata katiba mpya ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Inatoa majumuisho (usanisi) ya mapitio ya katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba za baadhi ya nchi zilizochaguliwa ambazo zimezingatia haki za mazingira, uhifadhi na menejimenti yake. Mapitio hayo yanadokeza uingizaji wa vipengele vya haki za mazingira, uhifadhi na manejimenti yake katika itakayokuwa - katiba mpya. Mada hii inatoa mapitio na mapendekezo juu ya nini kifanyike ili kuhakikisha kuwa

Mwongozo wa Katiba kwa Raia (toleo la tatu)

Nchi yetu iko kwenye mchakato wa kuandika Katiba mpya. Katiba iliyopo iliachwa na wakoloni waingereza ili itumike kwa muda wakati Katiba ya kudumu ikiandaliwa na watanzania wenyewe. Matarajio ya kuweza kuandaa mchakato wa kupata Katiba ya watanzania wenyewe hayajawahi kufanikiwa.

Ushindani wa Kodi Afrika ya Mashariki: Mbio za kuelekea chini, Motisha ya Kodi na Upotevu wa Mapato Tanzania?

Serikali ya Tanzania inatoa wigo mpana wa motisha wa kodi kwa wafanya biashara ili kuvutia viwango vikubwa zaidi vya uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje (FDIs) nchini. Utafiti huu unaonesha kuwa marupurupu ya kodi yanapelekea katika upotevu mkubwa wa mapato yasiyo ya lazima ili kuvutia na kudumisha uwekezaji wa nje. Kuona kitabu bofya hapa.

Je, Wewe ni Shujaa Katika Uangalizi wa Mafuta, Gesi Asilia na Madini?

Mapato ya serikali yanayotokana na sekta ya mafuta, gesi asilia na madini mara nyingi hufichwa na mwamvuli wa usiri unaotoa mwanya
wa kushamiri ufisadi na usimamizi mbaya. Kwa raia wa kawaida kufaidika, na nchi kukua, lazima taarifa zifichuliwe kuhusu kiasi gani cha
pesa kinazalishwa na kinaenda wapi. Uwazi kama huu wa mapato ni muhimu sana kwa wabunge ili kuhakikisha kuwa mapato yanatumika kwa faida ya majimbo yao, na kwa ujumla, nchi nzima. Kwa maelezo zaidi tafadhali bofya hapa.

Mwongozo wa Katiba kwa Raia (Toleo la pili)

Policy Forum imetoa toleo la pili la Mwongozo wa Katiba katika Jamii. Tafadhali angalia chapisho hapo chini. bofya hapa

Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2011- 2012

Bajeti ya Mwananchi ni bajeti iliyorahisishwa na ambayo imewekwa katika muundo unaomfanya mwananchi wa kawaida aweze kuelewa

Mgawanyo wa bajeti ya Sekta ya Kilimo: Je, nini hatma ya wakulima wadogo Tanzania?

Kama sekta ya kilimoTanzania itawekezwa ipasavyo ina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini. Kwa mujibu wa taarifa ya bajeti 2011/12 iliyotolewa na Waziri mwenye dhamana ya kilimo, kwa sasa sekta hii ina ajiri asilimia 77.5 ya watanzania na kuchangia asilimia 95 ya chakula kinachotumika nchini. Sekta ya kilimo pia inaonekana kukua kwa asilimia 4.2 tangu mwaka 2010 kutoka asilimia 3.2 ya mwaka uliotangulia.

Mgawanyo wa bajeti ya Sekta ya Kilimo: Je, nini hatma ya wakulima wadogo Tanzania?

Kama sekta ya kilimoTanzania itawekezwa ipasavyo ina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini. Kwa mujibu wa taarifa ya bajeti 2011/12 iliyotolewa na Waziri mwenye dhamana ya kilimo, kwa sasa sekta hii ina ajiri asilimia 77.5 ya watanzania na kuchangia asilimia 95 ya chakula kinachotumika nchini. Sekta ya kilimo pia inaonekana kukua kwa asilimia 4.2 tangu mwaka 2010 kutoka asilimia 3.2 ya mwaka uliotangulia.

Kwa nini afya siyo kipaumbele katika bajeti ya taifa 2011/12

Mchakato wa bajeti ya mwaka unatoa fursa ya kutathmini kama taarifa kwa umma kuhusu vipaumbele vya serikali vinafuatwa. Kwa mfano, katika miaka ya hivi karibuni serikali imeonyesha nia ya kutaka kupata thamani halisi ya fedha kadri inavyotoa bajeti yake ili kuweza kukabiliana na matumizi yasiyo ya lazima. Uchambuzi huu wa bajeti ya sekta ya afya 2011/12 kwa ufupi unatoa malengo maalumu yanayo tathmini thamani ya fedha. Uchambuzi unapima jinsi rasilimali zilizopo zimeweza kugawanywa na kama mgawanyo huo utaweza kuleta mabadiliko katika sekta ya afya.

Ijue Sheria Mpya ya Madini Namba 14 ya 2010

Sheria hii mpya ya madini imetungwa baada ya mchakato mrefu uliotanguliwa na Kamati na tume mbalimbali zilizoundwa pamoja na msukumo mkubwa kutoka asasi za kiraia na kuhitimishwa na Tume iliyoongozwa na Jaji Mstaafu Mark Bomani iliyoundwa mwaka 2007. Sheria hii inaweka utaratibu wa kisheria katika kutekeleza sera mpya ya madini ya mwaka 2009. Sheria hii ya madini namba 14 ya mwaka 2010 ilipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 23 Aprili 2010 na kusainiwa na Rais tarehe 20 Mei, 2010.

Ushawishi Bungeni Katika Tasnia ya Madini

Mwongozo huu umetolewa na Policy Forum katika jitihada zake za kurekodi yale yaliyojiri waliposhirikiana na wabunge katika kuchangia sheria mpya ya madini Tanzania, na kuboresha uwezo wa asasi za kiraia na vyombo vya habari katika kusimamia utendaji wa serikali kwenye sekta ya uziduaji (mafuta, gesi asilia na madini). Programu hii ilifanyika kwa ushirikiano na taasisi ya Revenue Watch. Kusoma zaidi tafadhali angalia viambatanisho hapo chini. bofya hapa

Utawala wa Kidemokrasia katika Jamii (5th Edition, 2011)

Mwananchi ana wajibu na majukumu yake kuhakikisha kuwa Kiongozi aliyemchagua au kuteuliwa anatimiza wajibu wake ipasavyo katika viwango vinavyokubalika katika eneo la kijiji/mtaa kulingana na mipango na makubaliano ya vikao vya kisheria vya kijiji na mtaa. Kila mwananchi ana wajibu wa kupinga na kukataa kila aina ya uovu katika jamii ikiwemo rushwa, uonevu, wizi, ubadhirifu wa mali za umma na ya watu binafsi. Kwa maelezo zaidi tafadhali angalia viambatanisho hapo chini.

Mwongozo wa Katiba kwa Raia

Kitabu cha Mwongozo wa Katiba kwa Raia” ni chapisho ambalo linatoa mchango katika mchakato mzima wa kupata Katiba mpya hapa nchini kwetu.
Madhumuni ya kitabu hiki ni kujenga na kuongeza uelewa wa watanzania juu ya Katiba, historia yake na mchakato wa uandikaji
wa Katiba hapa nchini na duniani. Dhumuni la pili ni kuwatoa hofu watanzania kuwa uandikaji wa Katiba si suala la wanasheria tu bali

TAFSIRI RAHISI YA MALENGO YA MKUKUTA II

2.0 USULI
MKUKUTA ni nini? Ni kifupisho cha maneno ya Kiswahili yenye maana ya Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania. Kuendelea kusoma bofya hapa

Utawala wa Kidemokrasia katika Jamii

Mwananchi ana wajibu na majukumu yake kuhakikisha kuwa Kiongozi aliyemchagua au kuteuliwa anatimiza wajibu wake ipasavyo katika viwango vinavyokubalika katika eneo la kijiji/mtaa kulingana na mipango na makubaliano ya vikao vya kisheria vya kijiji na mtaa. Kwa taarifa kamili tafadhali bofya hapa.

Makosa ya Rushwa katika Chaguzi Tanzania

Policy Forum na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) tunakuletea tena chapisho hili la pili katika mtiririko wa machapisho yanayohusu elimu kwa umma juu ya kupambana na rushwa.

Kuuelewa Mchakato Wa Bajeti Tanzania - Mwongozo Wa Jamii Za Kiraia

Bajeti kwa kawaida imekuwa ikichukuliwa kuwa ni kazi ya wataalamu, wachumi na wahasibu tu. Lakini uamuzi wa Serikali wa namna gani ya kukusanya mapato huwaathiri wananchi wote. Kiwango cha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na kodi nyingine huathiri bei za vitu vinavyotumiwa katika kaya.

Kuuelewa Mchakato wa Bajeti Tanzania - Mwongozo wa Jamii za Kiraia

Bajeti kwa kawaida imekuwa ikichukuliwa kuwa ni kazi ya wataalamu, wachumi na wahasibu tu. Lakini uamuzi wa Serikali wa namna gani ya kukusanya mapato huwaathiri wananchi wote. Kiwango cha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na kodi nyingine huathiri bei za vitu vinavyotumiwa katika kaya. Uamuzi wa matumizi ya serikali ndio huweka wazi iwapo viwango vya mishahara ya walimuna iwapo kutakuwa na dawa na vifaa vya kutosha katika zahanati au la.

TAMKO LA ASASI ZA KIRAIA JUU YA MAFANIKIO NA MADHARA KWA TANZANIA KUENDELEA KUTUMIA USHAURI WA IMF

Sisi wajumbe wa Asasi za kiraia za ki-Tanzania tuliokutana leo ukumbi wa Dar es Salaam International Conference Centre, tarehe 10 Machi 2009 kwa uratibu wa mtandao wa Policy Forum, Human Development Trust na Tanzania AIDs Forum, baada ya kujadili na kutafakari kwa kina taarifa za ''mafanikio'' ya utekelezaji mipango ya IMF na sera za Tanzania ki-uchumi kwa miaka ya 2000 hadi 2008 tumebaini yafuatayo:- 1.

Kuboresha Uwajibikaji wa Serikali za Mitaa: Fursa Ziko Waapi

Ni maslahi ya nani yanayozingatiwa wakati wa kupanga na kufanya maamuzi mengine? Kuna mikakati gani ya kuiwajibisha serikali katika utendaji wake? Tofauti nyingine ya muhimu ni kati ya uwajibikaji kwa jamii ama kwa ngazi za juu serikalini na wahisani. Kipeperushi hiki kinatoa muhtasari wa mchakato wa upangaji katika serikali za mitaa, na kinatoa mawazo juu ya namna Asasi za Kiraia na nyingine zinavyoweza kuongeza uwajibikaji wa serikali za mitaa kwa jamii.

Nioneshe Pesa Ziliko

Katika miezi ya hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko la madai ya uwajibikaji kutoka kwa Wabunge ambayo yamebadilisha muonekano wa Bunge na yamepelekea kujiuzuru kwa mawaziri kadhaa, ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu. Mswada wa Sheria ya Ukaguzi imepelekwa Bungeni chini ya hati ya dharura na itajadiliwa katika kikao kijacho cha Bajeti mwaka huu. Mswada huu unalenga kuiongezea Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAO) uhuru mkubwa wa kutoingiliwa na Dola katika utendaji wake wa kumsaidia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

UFAFANUZI WA MIKATABA YA MADINI TANZANIA

Zipo nyaraka nyingi zinazoonesha kuwa Tanzania imejaliwa madini mbalimbali yakiwamo almasi, dhahabu, na madini ya vito yasiyopatikana mahali pengine popote duniani, Tanzanite.

Hivi karibuni, sekta ya madini iliwekwa kwenye kipaumbele na Serikali ya Tanzania kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuchangia katika ukuaji wa haraka wa uchumi wa nchi.

Ripoti Ya Bomani - Taarifa Fupi Ya Kamati Ya Rais Ya Kuishauri Serikali Kuhusu Usimamizi Wa Sekta Ya Madini

Policy Forum tunayo furaha kuchapisha kitabu hiki ambacho kinatokana na ‘Taarifa ya Kamati ya Rais ya Kuishauri Serikali Kuhusu Usimamizi wa Sekta ya Madini’ Juzuu Namba 2.

Ripoti ya Bomani - Taarifa fupi ya Kamati ya Rais ya Kuishauri Serikali kuhusu Usimamizi wa Sekta ya Madini

Policy Forum tunayo furaha kuchapisha kitabu hiki ambacho kinatokana na ‘Taarifa ya Kamati ya Rais ya Kuishauri Serikali Kuhusu Usimamizi wa Sekta ya Madini’ Juzuu Namba 2.

Shukrani kwa Reginald Martin wa LHRC kwa ushirikiano wake wa hali na mali ikiwa ni pamoja na kutumia muda wake kuhakikisha anaihariri Taarifa hii fupi. Bila kumsahau mchora katuni wetu Nathan Mpangala.

Sera Gombo 2 Toleo 1 Aprili 2008

Mwanachama wa PF

Kwa ajili yako, hili ni toleo la kwanza la mwaka 2008 la jarida letu la SERA. Toleo hili linajadili matokeo muhimu ya mtandao kwa miezi mitatu ya mwanzo na pia nini kimepangwa na PF kwa mwaka huu kwa ujumla.

 Tafhadhali bofya hapa kufungua faili aina ya PDF ya toleo hili

Kufungua SERA kwa kiingereza, bofya hapa

Warsha Kuhusu Mpango Wa Kurekebisha Serikali Za Mitaa - Ripoti Ya Awali

Tarehe 26 na 27 Novemba 2007, Kikundi-kazi cha Serikali za Mitaa cha Policy Forum ikisaidiwa na Leadership Forum, kiliandaa warsha kuhusu mwelekeo wa Programu ya Kurekebisha Serikali za Mitaa kilichofanyika mji wa Kibaha. Dhumuni kuu lilikuwa kuwapa fursa maafisa wa TAMISEMI kutoa taarifa kwa wadau kutoka asasi mbalimbali kuhusu maendeleo ya programu hiyo.

Warsha kuhusu Mpango wa Kurekebisha Serikali za Mitaa - Ripoti ya Awali

Tarehe 26 na 27 Novemba 2007, Kikundi-kazi cha Serikali za Mitaa cha Policy Forum ikisaidiwa na Leadership Forum, kiliandaa warsha kuhusu mwelekeo wa Programu ya Kurekebisha Serikali za Mitaa kilichofanyika mji wa Kibaha. Dhumuni kuu lilikuwa kuwapa fursa maafisa wa TAMISEMI kutoa taarifa kwa wadau kutoka asasi mbalimbali kuhusu maendeleo ya programu hiyo. Vilevile, ilikuwa fursa kwa asasi kuwapa TAMISEMI maoni kuhusu programu inayofuata (2008 – 2013).

Prevention and Combating of Corruption Act 2007

Together with the Prevention and Combating of Corruption Bureau  (PCCB), Policy Forum Prevention this year published the popular version of the Prevention and Combating of Corruption Act 2007 (article 11) in Swahili entitled: IFAHAMU SHERIA MPYA YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA NCHINI NAMBA 11 YA MWAKA 2007.

The booklet is in pdf format click here to see the cover page and here to see the booklet

Jukwaa issue 3

This issue is on the topic of decentralisation. Where is Management of Public Money Most Accountable - at Central or Local level?. bofya hapa kuisoma

Jukwaa issue 4

Is Civil Society the Answer to Democracy and Accountability? kuisoma bofya hapa

Jukwaa issue 5

Should pregnant girls be expelled from school? Kuisoma bofya hapa

Jukwaa issue 2

Jukwaa Issue 2 focuses on the energy crisis gripping Tanzania. kuisoma bofya hapa

Jukwaa issue 1

The first issue of Jukwaa focuses on the subject of Constituency Development Funds

Marejeo ya Mkukuta

Social Media

We are on Facebook!


drupal hit counter