Sikika ni shirika lisilo la kiserikali, historia yake imeanza kutoka 1999. Shirika limebadilika kutoka kufanya kazi kwenye masuala yanayohusiana na vijana katika afya ya uzazi kuwa katika maeneo ya Utawala wa Afya na Fedha, Rasilimali Watu kwa Afya, Dawa na Tiba Vifaa na VVU na UKIMWI.
Mpango mkakati mpya wa miaka mitano (2019 - 2023) unaakisi ipasavyo mpango mkakati wa 2016 - 2020. Una mipango miwili, ambayo ni usimamizi wa fedha za umma na mpango wa afya.
Kazi zinazofanywa na Sikika:
Idara ya Usimamizi wa Fedha za Umma ilianzishwa mnamo 2016. Dhamira yetu kuu ni kukuza utawala bora wa kifedha kupitia utafiti katika kwenye sera, mchakato wa bajeti na matumizi ya umma.
Tunafanya uchechemuzi unaotegemea ushahidi - tunatumia utafiti kushawishi mabadiliko ya sera. Mkakati wetu wa utetezi unatokana na kuwasilisha matokeo na mapendekezo yetu kwa watunga sera wa Tanzania na kuboresha usambazaji wake kupitia njia mbalimbali kama vile muhtasari wa sera na mawasilisho mbalimbali.
Sikika inafanya kazi kuhakikisha kuna upatikanaji wa dawa bora na vifaa vya matibabu katika ngazi za kitaifa na wilaya.
Sikika inalenga kufikia malengo matatu mapana, ambayo ni kuongeza ufanisi wa bajeti, uwazi na pia kuboresha utendaji wa usimamizi katika ngazi ya kati na ya mitaa.