Tunaamini Vijana wana suluhisho la chagamoto mbalimbali za ulimwengu. Tumekuwa ni asasi inayojihusisha na maendeleo inayoongozwa na vijana nchini Tanzania kwa zaidi ya miaka 25, tukiwawezesha vijana ili waweze kupata riziki na kudai haki zao za kijinsia, na ili sauti zao zisikike.
Kazi zinazofanywa na Restless Tanzania:
Zaidi kuliko wakati wowote ule, ulimwengu unahitaji uongozi wa vijana kutatua changamoto zake kubwa. Restless Development Tanzania husaidia vijana kuwa viongozi na kuwawezesha kuonesha tija katika jamii na ulimwengu kwa ujumla. Kila mwaka Restless Tanzania hufundisha, kushauri, kulea na kuunganisha maelfu ya vijana kuongoza mabadiliko. Tumeweza kuwafikia vijana mbalimbali na kuwawezesha kwenya masuala ya ujasiriamali, ajira, usawa wa kijinsia na kuhusu maambukizi ya VVU.