Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum

Community Development for All (CODEFA) ni shirika lisilo la kiserikali linalofanya kazi ya kuboresha usawa na ustawi wa uchumi endelevu wa jamii za Tanzania Bara. CODEFA hufanya kazi ya kuongeza uelewa katika ngazi za chini na kuwezesha jamii kuchambua kwa kina hali zao, kutambua fursa na vizuizi kwa maendeleo, na kujipanga kwa pamoja  ili kujiletea maendeleo. Lengo kuu ni kuwezesha jamii zilizo pembezoni na zilizo katika mazingira magumu kushiriki kikamilifu katika kutokomeza umaskini.

Kazi zinazofanywa na CODEFA:

Fokasi ya CODEFA kwa mwaka 2021 hadi 2025 ni kuhusu ya utawala bora na demokrasia, uwajibikaji kwa jamii, usawa wa kijinsia na ulinzi wa watoto. Mkakati uliopo ni kuimarisha uwezo wa vikundi vya raia na asasi za kiraia katika maeneo ya ulinzi kwa jamii na uwajibikaji, haki za binadamu, uchechemuzi na uwezeshaji, na ufuatiliaji wa rasilimali za umma. Nia ni kuboresha uwezo wa vikundi vya pembezoni ili kutambua fursa zilizopo kwenye jamii zao na kuweza kutumia sayansi na teknolojia ili kujiletea maendeleo endelevu.

-6.9049279925472, 39.07152938671