Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum

Open Mind Tanzania (OMT) ni shirika lisilo la kiserikali linaloongozwa na vijana. Inashughulika na kufungua mawazo ya watu, vijana haswa kupitia uchechemuzi shirikishi na ujengaji uwezo katika maeneo ya uwezeshaji wa kisheria, kijamii, na kiuchumi, kuwawezesha (vijana) kuwa wasimamizi wa maendeleo yao na wachangiaji wakuu kwa ustawi wa jamii yao , nchi na ulimwengu kwa jumla. 

Shirika lilianzishwa mnamo Juni 2006 na dhamira ya kuhakikisha kuwa watu wana uelewa mzuri wa matakwa ya vijana na mahitaji ya maendeleo, kama vile hitaji la ujuzi wa biashara na maendeleo ya ujasiriamali; hitaji la ujuzi wa kuajiriwa, upatikanaji wa kazi zenye heshima, haki za binadamu, haki za raia na majukumu, demokrasia na utawala bora, maswala ya uchumi na msaada wa kisheria.

Kazi zinazofanywa na OMT:

OMT ni miongoni mwa mashirika ya maendeleo yanayoongozwa na vijana na yanayolenga vijana nchini Tanzania katika kuunda mazingira wezeshi ya kuboresha maisha ya vijana wa kiume na wa kike ikiwa ni pamoja na kukuza ushiriki wao katika michakato ya maendeleo. 

Programu za OMT zimejikita katika Maeneo ya Matokeo muhimu ya kimkakati:

a. Kuimarisha Uwezo wa Taasisi & Ujasilimali; 

b. Kuongezeka kwa Upataji wa Ajira kwa Vijana; Ujasiriamali na Ubunifu; 

c. Kuwawezesha Vijana Kushawishi Sera na Programu za Maendeleo; 

d. Kuongezeka kwa Upatikanaji wa Haki za Binadamu kwa Vijana na Watoto  

e. Kukuza Ujumuishaji na Uwezeshaji na Mitandao

-6.8083836303095, 39.282221702912