Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum

Norwegian Church Aid (NCA) ilianzishwa nchini Tanzania mnamo 2006 na ina historia ndefu ya kufanya kazi pamoja na wahusika wa kidini kusaidia watu kujikwamua kutoka kwenye umaskini na kukuza haki. Wakati wote wa uwepo wake, NCA imeendeleza harakati za vyama vya kijamii, ikifanya kazi kwa amani na mshikamano wa kijamii, utawala unaowajibika, haki ya kiuchumi na usawa wa kijinsia. Kwa NCA, kuwezesha mazungumzo na ushirikiano wa wadau wengi ni njia muhimu ya kuimarisha jukumu la asasi za kiraia na kukuza matokeo ya maendeleo endelevu nchini.

NCA nchini Tanzania inaimarisha uwezo wa watendaji wa asasi za kiraia na nafasi ya kiraia kukuza utu na haki za binadamu, na kuwapa watu uwezo wa kushiriki katika maendeleo na utekelezaji wa sera za umma na mipango ya maendeleo. Pamoja na asasi nyingine za kiraia, NCA na washirika wake wanafanya kazi kutekeleza mipango ya maendeleo ya muda mrefu katika maeneo yafuatayo:

a. Kupambana na Ukosefu wa usawa 

b. Uwezeshaji wa Kiuchumi

c. Ukatili wa Kijinsia 

-6.7635662951085, 39.255695569551