Tanzania Youth Vision Association (TYVA) ni shirika linaloongozwa na vijana, lisilo la kifaida na lisilo la kiserikali na la wanachama lililoanzishwa mnamo 29 Julai 2000 na kusajiliwa na nambari ya usajili (00NGO / R2 / 000425) kufanya kazi kama Shirika lisilo la kiserikali linaloangazia uhamasishaji wa vijana na uwezeshaji. TYVA inafafanua ujana kuwa na umri wa miaka 16-30.
Kazi zinazofanywa na TYVA:
Shule ya TYVA
Huu ni mpango wa kuwajengea uwezo vijana, hivi karibuni wanachama wa TYVA wamekuwa wanufaika wa mpango huu. TYVA hufanya kazi ya uchechemuzi, uchambuzi wa Sera, upangaji miradi na usimamizi, mawasiliano kwa umma, ujuzi wa kutafuta fedha, uandishi wa pendekezo na utatuzi wa migogoro.
Majadiliano ya Dira
Majadiliano ya Dira ni majukwaa yanayotumiwa na TYVA kutetea sera za vijana na maswala mengine muhimu yanayohusu ustawi wa Taifa. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2000, TYVA imetumia mazungumzo ya Dira kutetea ushiriki mzuri wa vijana katika mijadala na majadiliano ya kitaifa.
Ilani ya Vijana
Huu ni mpango unaoratibiwa na TYVA kwa kushirikiana na mashirika mengine yanayoongozwa na vijana.