Website
TNRF iliundwa mwaka 2021 kama Kikundi Kazi cha Wanyamapori (WWG) na kikundi kidogo cha watu walikuwa na dhamira yenye mrengo wa haki kwa ajili ya kutatua changamoto zilizokuwa zinaikumba sekta ya maliasili nchini.
Mrengo huo ulikuwa na shauku ya kuona changamoto zinazokabili sekta ya maliasili zikitatuliwa kwa umoja na siyo utengano. Mfano ili kuweza kukabiliana na changamoto za maliasili kuna haja ya kuoanisha na kuangalia sekta nyingine kama vile misitu, uvuvi, wanyamapori na wanyama wafugwao (uchungaji wa wanyama).