Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum

HakiMadini ilianza baada ya athari zilizokuwa zinajitokeza za matukio ya ukiukwaji wa Haki za Binadamu katika maeneo ya uziduaji miaka ya 1990. Hasa katika maeneo ya uchimbaji wa Tanzanite, Mererani. Shughuli za mwanzo zilihusu kutetea haki za watoa huduma ili waweze kufanya biashara katika maeneo ya migodi pamoja na kufanya kazi kwa karibu na Serikali kutatua migogoro iliyokuwepoo hasa ule wa wachimbaji wadogo na kampuni ya Tanzanite One.

Hata hivyo iligundulika migodi mingi nchini ilikuwa inakumbana na tatizo kama la Mererani. Mfano katika mgodi wa Bulyanhulu kulikuwa na tatizo la kufukuzwa kwa wachimbaji wadogo zaidi ya 200,000 na ardhi yao ikachukuliwa na mchimbaji mkubwa kutoka Canada.

Wigo wa utendaji kazi wa HakiMadini umeendelea kukuwa kwa kasi ukiangazia zaidi hali tete katika migodi, siyo tu kwa kukabiliana na madhara yanayotokana na uwekezaji kutoka nje na sera ya madini bali pia kwa kushirikiana kutatua changamoto zilizojikita katika jammii kama vile HIV, matukio ya kinyanyasaji katika familia na kutoa njia mbadala za kuboresha uchumi na maisha kwa ujumla.

-3.3591320760687, 36.659690615342