Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum

Lawyers’ Environmental Action Team (LEAT) ni asasi isiyo ya kiserikali na isiyo jiendesha kwa faida inayojishughulisha na usimamizi na ulinzi wa mazingira nchini Tanzania. LEAT imejikita katika shughuli za utafiti katika usimamizi wa maliasili haswa katika ardhi, madini, wanyamapori, rasilimali za maji na misitu. LEAT inajishughulisha na kutetea marekebisho ya kisheria na sera katika utunzaji wa mazingira na usimamizi wa maliasili. LEAT inashiriki zaidi katika kukuza uelewa kwa jamii za mitaa na mawakala wa serikali kuhusu umuhimu wa kuzingatia kanuni bora za usimamizi wa mazingira na maliasili.

Hizi ni baadhi ya kazi zinazofanywa na LEAT:

Tangu kuanzishwa kwake, LEAT imejitambulisha kama shirika linaloongoza la sheria ya mazingira ya masilahi ya umma, haswa katika maeneo ya uziduaji, wanyamapori, na usimamizi mpana wa mazingira.

Tangu kuundwa kwake, LEAT imechapisha majarida kadhaa, miongozo ya mafunzo, na ripoti juu ya usimamizi wa maliasili, haki za binadamu, na mazingira. LEAT imechangia michakato ya mageuzi ya sera na sheria, pamoja na kutungwa kwa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira 2004, Sheria ya Usimamizi wa Maafa 2014, marekebisho ya Sheria ya Madini ya 2010, Sheria ya Maliasili na Rasilimali ya 2017

Kwa mwaka 2019, LEAT ilifanya kazi kwa: (a) kuongeza maarifa juu ya tasnia ya uziduaji sheria na sera nchini Tanzania na mataifa mengine ya Afrika Mashariki (b) uwazi katika ukusanyaji, uokoaji, uwekezaji na matumizi ya mapato ya mafuta na gesi; (c) kuongeza uwezo wa wanasheria wa Tanzania kujadili Makubaliano ya Uendelezaji Madini (MDAs) na Makubaliano ya Mgawanyo waUzalishaji (PSAs).

-6.7578367463716, 39.2428442677