Skip to main content

Ripoti Fupi Ya Uchambuzi Wa Bajeti Ya Wizara Ya Nishati Na Madini Kwa Mwaka 2017/2018

Imechapishwa na Policy Forum

Sekta ya nishati inakabiliwa na changamoto mbalimbali hapa nchini ikiwemo: upungufu wa fedha za kutosha, ushiriki na uwekezaji mdogo wa sekta binafsi katika miradi mikubwa ya nishati; utegemezi mkubwa sana kwa tungamotaka kama chanzo cha nishati; gharama kubwa za tozo za uunganishaji na usambazaji wa umeme; upungufu wa wataalam na tafiti; uwepo na matumizi ya teknolojia miundombinu duni; na uwekezaji mdogo katika nishati jadidifu. Soma zaidi...

Viwango vya Utawala Bora na Usimamizi wa Rasilimali Asilia (RGI) hutathmini jinsi nchi zenye utajiri wa rasilimali za Mafuta, Gesi na Madini zinavyojisimamia

Imechapishwa na Policy Forum

Sekta ya Mafuta na Gesi asilia ina alama 53 kati ya alama 100 za RGI 2017. Tofauti na sekta ya madini ambayo ni kongwe, Tanzania bado haijaanza uzalishaji mkubwa wa gesi baada ya ugunduzi wa gesi nyingi katika kina kirefucha bahari ya Hindi  ambayo hivi sasa inakadiriwa kuwa futi za ujazo trilioni 57. Hali ya kuridhisha ya Tanzania katika uwezekano wa kupata thamani ya rasilimali, kipengele kinachopima ubora wa utawala katika utoaji wa leseni, mfumo wa kodi, athari kwa jamii na ushiriki wa Serikali, hutegemea sana utaratibu wa kisheria wenye masharti mahimu kuhusu utawala na uwazi.

Kuelekea Uwajibikaji Endelevu Katika Usimamizi Wa Maliasili Nchini Tanzania

Imechapishwa na Policy Forum

Siku chache zilizopita, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli aliunda kamati mbili za wataalamu kwa ajili ya kuchunguza taarifa za kuwapo kwa udanganyifu wa kiwango cha madini katika mchanga wa dhahabu (makinikia), ambao umekuwa ukisafirishwa kupelekwa nje ya nchi. Mchanga huo ni ule unaotoka katika migodi ya dhahabu ya Bulyanhulu na Buzwagi ambayo kwa pamoja inamilikiwa na Kampuni ya Acacia.

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari: Uzinduzi wa Ripoti ya Hali ya Utekelezaji wa Dira ya Madini ya Afrika

Imechapishwa na Policy Forum

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UZINDUZI WA RIPOTI YA HALI YA UTEKELEZAJI WA DIRA YA MADINI YA AFRIKA

Policy Forum kwa kushirikiana na Tax Justice Network – Africa (TNJ-A), Tanzania Tax Justice Coalition (TTJC) na HakiRasilimali wameandaa uzinduzi wa kitaifa wa Ripoti ya Hali ya Utekelezaji wa Dira ya Madini ya Afrika (AMV) utakaofanyika katika ukumbi wa Bunge (Old Dispensary Hall), Dodoma  tarehe 15 Mei, 2017.  Uzinduzi  huo utaanza saa 6:30 mchana.

Hotuba Iliyotolewa Na Kamishna Wa Madini, Wizara Ya Nishati Na Madini, Katika Ufunguzi Wa Mkutano Wa Indaba 2016, Tarehe 26 Oktoba 2016 Kwenye Ukumbi Wa Kimataifa Wa Julius Nyerere Jijini Dar Es Salaam

Imechapishwa na Policy Forum

Waandaaji wa Kongamano la TAEI (INDABA) 2016,

Watoa mada waliokaribishwa kutoka maeneo mbalimbali Afrika,

Makundi ya madhehebu,

Wawakilishi wa Mashirika ya vyama vya Kijamii,

Wataalamu,  

Washirika wa kimaendeleo,

Wageni waalikwa,  

Mabibi na mabwana,

Habari za asubuhi?

Miswada Kuhusu Tasnia Ya Uziduaji: Msimamo Wa Kikundi Kazi Cha Azaki Zinazoshiriki Kwenye Tasnia Ya Uziduaji

Imechapishwa na Policy Forum

Tarehe 16 Juni 2015 Serikali ya Tanzania  ilipeleka miswada mitatu bungeni inayohusu sekta ya uziduaji chini ya “Hati ya Dharura.”  Miswada hiyo ni Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji Katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia ya mwaka 2015 (The Tanzania Extractive Industries (Transparency and Accountability) Act 2015, Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi ya mwaka 2015. (The Oil and Gas Revenue Management Act 2015)  Sheria ya Petroli ya mwaka 2015 (The Petroleum Act 2015).

Kuvuja kwa mkataba wa Statoil kunadhihirisha kuwa usiri unavunja imani

Imechapishwa na Policy Forum

Kufuatia ugunduzi wa  uhakika wa hivi karibuni wa gesi  asilia Tanzania, nchi imejitokeza kuwa na uwezekano mkubwa wa uzalishaji gesi kwa kiwango cha juu katika Afrika ya Mashariki, na kuleta hamasa miongoni mwa  wananchi, jumuiya za kiraia, na wanasiasa kuhusu  matarajio ya  rasilimali  hiyo kuchochea maendeleo ya taifa .  Serikali,  inaaminika,  imeanza mchakato  wa kuandaa sera na miundo ya kisheria zitakazosaidia usimamizi  wa  uchunguzi, uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa gesi asilia.

Mdahalo wa Asubuhi wa Policy Forum wa Jinsi ya Kufaidika na Gesi:Jinsi ya Kuimarisha Ushiriki wa Wananchi Tanzania

Imechapishwa na Policy Forum

Pamoja na kupatikana  na hifadhi ya gesi Tanzania , kumekuwa na majadiliano wa kutosha ya jinsi  uchimbaji wa rasilimali hii unaweza kuboreshwa ili  uweze kuwanufaisha wananchi nchini . Wadau wametoa wito kwa Serikali kuonyesha dhamira itakayoweza kuelekea kuimarisha ushiriki wa wananchi (local content) katika sekta ya madini na makampuni ya mafuta na gesi ya kimataifa kuonyesha hatua madhubuti itakazochukua juu ya hili ikiwa ni pamoja na maendeleo ya rasilimali watu .

Subscribe to Extractive Industry