Pamoja na kupatikana na hifadhi ya gesi Tanzania , kumekuwa na majadiliano wa kutosha ya jinsi uchimbaji wa rasilimali hii unaweza kuboreshwa ili uweze kuwanufaisha wananchi nchini . Wadau wametoa wito kwa Serikali kuonyesha dhamira itakayoweza kuelekea kuimarisha ushiriki wa wananchi (local content) katika sekta ya madini na makampuni ya mafuta na gesi ya kimataifa kuonyesha hatua madhubuti itakazochukua juu ya hili ikiwa ni pamoja na maendeleo ya rasilimali watu .
Kuchangia zaidi kwa mjadala huu, Policy Forum waliandaa mdahalo wa asubuhi(breakfast debate) unaohusiana na maada hii na waliwaalika Statoil , kampuni inayoongoza katika uzalishaji wa mafuta na gesi , ili kuweza kujadili mbinu zao za kimkakati za ushiriki wa wananchi.
Statoil ina nia ya kuchangia na kuweka kumbukumbu za maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika nchi ambapo inafanya kazi kwa njia ya ununuzi wa ndani, ajira za ndani za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja, maendeleo ya miundombinu ya ndani, maendeleo ya uwezo na uwekezaji jamii .
Akizungumza katika mdahalo huo ambao ulifanyika tarehe 25 Aprili 2014 katika ukumbi wa British Council, Dar es Salaam , Bw Harald Back , Meneja wa kampuni ya Statoil alisema kwamba mkakati wa usiriki wa wananchi wa Statoil unaruhusu wauzaji wa ndani katika nchi 35 inapofanya kazi (ambayo ni pamoja na Tanzania ) kushindana na hutumiwa na kampuni ya kujadiliana na serikali juu ya baadhi ya masuala yanayohusiana na mafuta na uzalishaji wa gesi .
Alisema Statoil ina nia ya "local content" katika shughuli zake na kwa njia ya usambazaji wake ambapo ushiriki wa wananchi ni sehemu muhimu ya mkakati wake wa manunuzi. Akaongeza kwa kusema kwamba mchakato wa Statoil wa zabuni ni wa wazi, Local Content imewekwa sehemu ya mchakato wake wa tathmini na kwamba miundo ya mkataba inakuwa na fursa zinazopelekea ushiriki wa wananchi.
Alihitimisha kwa kusema kwamba kiwango cha juu cha ushiriki wa wananchi kitahitaji mbinu za ushirikiano kuundwa na serikali ya Tanzania .
Mchangiaji wa mdahalo huo Neema Lugangira Apson , Mtaalam wa Local Content ambaye hivi karibuni ilizindua kitabu chake kiitwacho: "Local Content in Supply Development" ambacho kwa sasa kinasambazwa ili kukuza uelewa wa mafuta na gesi na maandalizi kwa ajili ya maendeleo ya wasambazaji. Kitabu kinasema kwamba Watanzania watafaidika kiuchumi na kijamii na sekta hii kama watafahamishwa juu ya faida ikiwa ni pamoja na kuongeza uwezo wa wauzaji wa ndani .
Search
Upcoming Events
There is no upcoming events.
If you have any feedback or you would like to obtain policies related materials, please reach us through:
- P.O. BOX 38486, Dar es Salaam
- (+255) 782 317 434
- info@policyforum.or.tz