Warsha ya Asasi za Kiraia Juu ya Viwango Vipya vya Mpango wa Uwazi wa Tasnia ya Uziduaji (EITI)
Policy Forum kwa kushirikiana na Mpango wa Uhamasishaji Uwazi katika Mapato ya Madini, Gesi asilia na Mafuta Tanzania ( TEITI ) pamoja na Hakimadini wameandaa warsha ( 2-3 Aprili 2014) Arusha kwa lengo la kuwawezesha wawakilishi wa asasi za kiraia za kaskazini mwa Tanzania zinazofanya kazi katika masuala ya uziduaji kuongeza uelewa wao wa viwango vipya vya Mpango wa Uhamasishaji Uwazi katika Mapato ya Madini au Mpango wa Uwazi katika Tasnia ya Uziduaji (EITI) ili kuongeza uwezo wao wa kuiwajibisha serikali yao.