Skip to main content

Risala ya Kumkaribisha Mgeni rasmi Mhe . Mohamed Omary Mchengerwa (MB), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Katika Hafla ya Uzinduzi wa Kitabu cha MWELEKEO WA KATIBA MPYA TANZANIA: Tulikotoka, Tulipo na Tuendako.

Imechapishwa na Policy Forum

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe Omary Mchengerwa (MB)

Waheshimiwa Wabunge

Ndugu Mwenyekiti wa Bodi ya PF Bw Bakari Khamis Bakari

Ndugu Wajumbe wa Bodi ya PF

Ndugu Viongozi na watendaji wa AZAKI hasa wajumbe wa Kikundi Kazi cha Serikali za Mitaa cha Policy Forum

Ndugu Mratibu wa Policy Forum, Bw Semkae Kilonzo

Ndugu waandishi wa habari,

Ndugu Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana

Bajeti ya Elimu ya Mwaka 2016/2017: Je, ni Kweli Imeongezeka?

Imechapishwa na Policy Forum

Katika bajeti ya mwaka 2016/2017 Serikali iliidhinisha jumla ya Shilingi Bilioni 4,770 kwa matumizi ya sekta ya Elimu zikiwa zimejumuisha matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi. Kiasi hiki ni sawa na asilimia 22.1 ya jumla ya bajeti yote ya Taifa ambayo ni Shilingi Bilioni 29,539.6. Takwimu hizi hazijumuishi deni la taifa. Kusoma zaidi bofya hapa.

Hotuba Iliyotolewa Na Kamishna Wa Madini, Wizara Ya Nishati Na Madini, Katika Ufunguzi Wa Mkutano Wa Indaba 2016, Tarehe 26 Oktoba 2016 Kwenye Ukumbi Wa Kimataifa Wa Julius Nyerere Jijini Dar Es Salaam

Imechapishwa na Policy Forum

Waandaaji wa Kongamano la TAEI (INDABA) 2016,

Watoa mada waliokaribishwa kutoka maeneo mbalimbali Afrika,

Makundi ya madhehebu,

Wawakilishi wa Mashirika ya vyama vya Kijamii,

Wataalamu,  

Washirika wa kimaendeleo,

Wageni waalikwa,  

Mabibi na mabwana,

Habari za asubuhi?

Mjue Diwani (Toleo la Tatu)

Imechapishwa na Policy Forum

Ndugu msomaji, tunayo furaha kukuletea kitabu kipya kiitwacho “Mjue Diwani” ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wetu wa Kikundi Kazi cha Serikali za Mitaa wa kuwaelimisha wananchi kuhusu utawala wa Serikali za Mitaa na
kukuza uwajibikaji katika jamii.

Malengo Ya Maendeleo Endelevu Na Wajibu Wa Serikali Za Mitaa

Imechapishwa na Policy Forum

Ndugu Msomaji, tunafurahi kwa mara nyingine kukuletea kitabu kipya kiitwacho “Malengo ya Maendeleo Endelevu na Wajibu wa Serikali za Mitaa” ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wa Kikundi Kazi cha Serikali za Mitaa cha Jukwaa la Sera (PF-LGWG) kwa kuelimisha wananchi kuhusu sera za kitaifa na kimataifa zinazopaswa kutekelezwa na Serikali za Mitaa ili kuhamasisha ushiriki wa
wananchi kwenye masuala ya umma na kukuza uwajibikaji katika jamii.

Maazimio Na Mapendekezo Ya Waheshimiwa Madiwani Baada Ya Kushiriki Mafunzo Ya Uongozi Na Uwajibikaji Wa Kijamii

Imechapishwa na Policy Forum

Sisi Waheshimiwa madiwani tulioshiriki warsha ya mafunzo ya uongozi na uwajibikaji wa kijamii iliyoandaliwa na kuratibiwa na Kinkundi kazi cha Serikali za Mitaa cha Policy Forum kwa kushirikiana na halmashauri ya Kiteto kati ya tarehe 18 hadi 23 Julai 2016,

Baada ya kupokea na kujadili mada mbalimbali, tumetambua umuhimu wa nyaraka na taarifa mbalimbali kwenye hatua zote za usimamizi wa rasilimali za umma na mfumo wa uwajibikaji jamii,

Taarifa ya Ufuatiliaji wa Uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Oktoba 25, 2015

Imechapishwa na Policy Forum

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kwa kushirikiana na Policy Forum, ilifuatilia mchakato wa uchaguzi mkuu wa Tanzania wa mwaka 2015 katika mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Mwanza. Lengo kuu la ufuatiliaji huo lilikuwa ni kutathimini uzingatiaji wa misingi ya kidemokraisa, haki za binadamu, na utawala bora kwenye mchakato mzima wa uchaguzi mkuu wa 2015. Kusoma zaidi bofya hapa.

Tangazo la Kifo: Mungu Akulaze Mahali Pema Peponi Alex Modest Ruchyahinduru

Imechapishwa na Policy Forum

Sekretariati ya Policy Forum inasikitika  kutangaza kifo cha Alex Modest Ruchyahinduru, meneja wetu wa Mawasiliano na Uchechemuzi, aliyefariki asubuhi ya leo Mei Mosi 2016 katika hospitali ya Aga Khan mjini Dar es Salaam. Baadhi yenu huenda mlikuwa na taarifa za kulazwa kwake kufuatia operesheni ya kichwa iliyofanyika kipindi cha Pasaka takriban mwezi mmoja uliyopita. Alex alijiunga na Policy Forum Machi 2009.

Subscribe to Resources