Mtazamo wa Azaki Kuhusu Siku 100 za Magufuli Madarakani
Kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, 2015, Asasi Za Kiraia (AZAKI) chini ya Kikundi Kazi cha Bajeti cha Policy Forum ziliandaa na kuwasilisha kijarida kinachoitwa“Vipaumbele Vyetu Vikuu kwa Serikali Ijayo” kwa vyama mbalimbali vya siasa vilivyokuwa vinashiriki katika uchaguzi ili kutilia mkazo yaliyomo kwenye kijitabu hicho. Kijarida hicho kilikuwa na masuala nyeti yaliyohitaji serikali ya awamu ya tano kuzingatia.