Skip to main content

Kuelekea Uwajibikaji Endelevu Katika Usimamizi Wa Maliasili Nchini Tanzania

Imechapishwa na Policy Forum

Siku chache zilizopita, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli aliunda kamati mbili za wataalamu kwa ajili ya kuchunguza taarifa za kuwapo kwa udanganyifu wa kiwango cha madini katika mchanga wa dhahabu (makinikia), ambao umekuwa ukisafirishwa kupelekwa nje ya nchi. Mchanga huo ni ule unaotoka katika migodi ya dhahabu ya Bulyanhulu na Buzwagi ambayo kwa pamoja inamilikiwa na Kampuni ya Acacia.

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari: Uzinduzi wa Ripoti ya Hali ya Utekelezaji wa Dira ya Madini ya Afrika

Imechapishwa na Policy Forum

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UZINDUZI WA RIPOTI YA HALI YA UTEKELEZAJI WA DIRA YA MADINI YA AFRIKA

Policy Forum kwa kushirikiana na Tax Justice Network – Africa (TNJ-A), Tanzania Tax Justice Coalition (TTJC) na HakiRasilimali wameandaa uzinduzi wa kitaifa wa Ripoti ya Hali ya Utekelezaji wa Dira ya Madini ya Afrika (AMV) utakaofanyika katika ukumbi wa Bunge (Old Dispensary Hall), Dodoma  tarehe 15 Mei, 2017.  Uzinduzi  huo utaanza saa 6:30 mchana.

Maelezo ya Ripoti ya Mbeki Kuhusu Uhamishaji Haramu wa Fedha kutoka Barani Afrika

Imechapishwa na Policy Forum

Februari 2015 Jopo la Ngazi ya Juu Kuhusu Uhamishaji Haramu wa Fedha kutoka Barani Afrika, likiongozwa na Mwenyekiti wake Rais Thabo Mbeki, liliwasilisha ripoti yake kwa Tume ya Umoja wa Afrika/Tume ya Umoja wa Kimataifa ya Kiuchumi Barani Afrika (AUC/ECA). Ripoti ilionesha kuwa nchi za Kiafrika hupoteza kwa wastani dola bilioni 50 kwa mwaka kutokana na uhamishaji haramu wa fedha. Shughuli za kibiashara za sekta binafsi ndizo zinazochangia kwa kiwango kikubwa uhamishaji haramu wa fedha (IFFs), zikifuatiliwa na uhalifu uliopangwa, kisha shughuli za sekta ya umma.

Risala ya Kumkaribisha Mgeni rasmi Mhe . Mohamed Omary Mchengerwa (MB), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Katika Hafla ya Uzinduzi wa Kitabu cha MWELEKEO WA KATIBA MPYA TANZANIA: Tulikotoka, Tulipo na Tuendako.

Imechapishwa na Policy Forum

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe Omary Mchengerwa (MB)

Waheshimiwa Wabunge

Ndugu Mwenyekiti wa Bodi ya PF Bw Bakari Khamis Bakari

Ndugu Wajumbe wa Bodi ya PF

Ndugu Viongozi na watendaji wa AZAKI hasa wajumbe wa Kikundi Kazi cha Serikali za Mitaa cha Policy Forum

Ndugu Mratibu wa Policy Forum, Bw Semkae Kilonzo

Ndugu waandishi wa habari,

Ndugu Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana

Bajeti ya Elimu ya Mwaka 2016/2017: Je, ni Kweli Imeongezeka?

Imechapishwa na Policy Forum

Katika bajeti ya mwaka 2016/2017 Serikali iliidhinisha jumla ya Shilingi Bilioni 4,770 kwa matumizi ya sekta ya Elimu zikiwa zimejumuisha matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi. Kiasi hiki ni sawa na asilimia 22.1 ya jumla ya bajeti yote ya Taifa ambayo ni Shilingi Bilioni 29,539.6. Takwimu hizi hazijumuishi deni la taifa. Kusoma zaidi bofya hapa.

Hotuba Iliyotolewa Na Kamishna Wa Madini, Wizara Ya Nishati Na Madini, Katika Ufunguzi Wa Mkutano Wa Indaba 2016, Tarehe 26 Oktoba 2016 Kwenye Ukumbi Wa Kimataifa Wa Julius Nyerere Jijini Dar Es Salaam

Imechapishwa na Policy Forum

Waandaaji wa Kongamano la TAEI (INDABA) 2016,

Watoa mada waliokaribishwa kutoka maeneo mbalimbali Afrika,

Makundi ya madhehebu,

Wawakilishi wa Mashirika ya vyama vya Kijamii,

Wataalamu,  

Washirika wa kimaendeleo,

Wageni waalikwa,  

Mabibi na mabwana,

Habari za asubuhi?

Mjue Diwani (Toleo la Tatu)

Imechapishwa na Policy Forum

Ndugu msomaji, tunayo furaha kukuletea kitabu kipya kiitwacho “Mjue Diwani” ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wetu wa Kikundi Kazi cha Serikali za Mitaa wa kuwaelimisha wananchi kuhusu utawala wa Serikali za Mitaa na
kukuza uwajibikaji katika jamii.

Subscribe to Resources