Miswada Kuhusu Tasnia Ya Uziduaji: Msimamo Wa Kikundi Kazi Cha Azaki Zinazoshiriki Kwenye Tasnia Ya Uziduaji
Tarehe 16 Juni 2015 Serikali ya Tanzania ilipeleka miswada mitatu bungeni inayohusu sekta ya uziduaji chini ya “Hati ya Dharura.” Miswada hiyo ni Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji Katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia ya mwaka 2015 (The Tanzania Extractive Industries (Transparency and Accountability) Act 2015, Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi ya mwaka 2015. (The Oil and Gas Revenue Management Act 2015) Sheria ya Petroli ya mwaka 2015 (The Petroleum Act 2015).