Muhtasari wa Ripoti: Ukusanyaji wa Mapato ya Ndani Kwenye Sekta ya Uziduaji Unavyoweza Kufadhili Mabadiliko ya Tabianchi
Kama ilivyo kwa nchi nyingi zinazoendelea, Tanzania imeathiriwa sana na mabadiliko ya tabianchi, madhara ambayo hayaishii tu kusababisha mafuriko na ukame lakini yanaharibu miundombinu na hata kuathiri maisha ya watanzania kwani kilimo, sekta inayoajiri watu wengi takriban asilimia 65.5 imeathiriwa sana na hali mbaya ya mvua. Aidha, athari za mabadiliko ya tabianchi pia zimeathiri sekta ya uziduaji hususan ufanisi katika shughuli za Uchimbaji mkubwa na mdogo wa madini (Large- & Small-scale mining operations).