Wananchi Wahimizwa Kuchukua Nafasi ya Uongozi Wahimizwa Kushiriki Katika Maamuzi ya Maendeleo Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika
Mdahalo wa wa asubuhi chini ya mradi wa Raia Makini ulifanyika tarehe 17 Novemba 2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, mkoani Katavi. Lengo kuu lilikuwa kuangazia umuhimu wa ushiriki wa wananchi katika upangaji wa mipango na bajeti, pamoja na namna Halmashauri inavyotarajia kuwawezesha wananchi kushiriki katika mchakato wa bajeti.