Mapitio ya " Suala la Dola Bilioni Moja": Tanzania Inaendelea Kupoteza Kiasi Gani cha Fedha za Kodi?
Serikali inalo jukumu kubwa la kuwahakikishia na kuwapatia watu wake huduma na bidhaa za umma. Hizi ni pamoja na afya, elimu, maji, miundombinu, ulinzi na usalama na kadhalika. Huduma na bidhaa hizi ni muhimu sana ili wananchi waweze kustawi na kuondokana na matatizo kama vile umaskini, ujinga na maradhi.Huduma na bidhaa za umma hugharimu rasilimali nyingi zikiwemo fedha. Fedha hizi ni za kutoka ndani na nje ya nchi. Fedha za ndani ni pamoja na mapato ya kikodi na yasiyo ya kikodi.