Skip to main content

Muhtasari wa Ripoti: Ukusanyaji wa Mapato ya Ndani Kwenye Sekta ya Uziduaji Unavyoweza Kufadhili Mabadiliko ya Tabianchi

Imechapishwa na Policy Forum

Kama ilivyo kwa nchi nyingi zinazoendelea, Tanzania imeathiriwa sana na mabadiliko ya tabianchi, madhara ambayo hayaishii tu kusababisha mafuriko na ukame lakini yanaharibu miundombinu na hata kuathiri maisha ya watanzania kwani kilimo, sekta inayoajiri watu wengi takriban asilimia 65.5 imeathiriwa sana na hali mbaya ya mvua. Aidha, athari za mabadiliko ya tabianchi pia zimeathiri sekta ya uziduaji hususan ufanisi katika shughuli za Uchimbaji mkubwa na mdogo wa madini (Large- & Small-scale mining operations).

Mikataba ya utozaji kodi mara mbili (DTAs) na hatma yake kwa nchi

Imechapishwa na Policy Forum

Mwaka 2018 Policy Forum (PF) mtandao wa asasi zaidi ya 70 zilizosajiliwa Tanzania ilichapisha utafiti unaohusu mikataba ya utozaji kodi mara mbili (Double Taxation Agreements - DTAs) kati ya Tanzania na Afrika Kusini na Tanzania na India. Makala hii ni tafsiri ya muhtasari wa utafiti huo ambao ulitumika kwenye kikao cha pamoja na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao wapo kwenye Mtandao wa Kupambana na Rushwa (APNAC) mnamo Novemba 8, 2018 Jijini Dodoma.

Utozaji Kodi kwa Miji Inayokuwa Tanzania: Ukusanyaji wa Kodi ya Majengo kati ya Serikali Kuu na Mamlaka za Serikali za Mitaa

Imechapishwa na Policy Forum

Ufanisi wa mfumo wowote ule wa kukusanya kodi za majengo unahitaji ushirikiano imara kati ya Mamlaka ya Ukusanyaji wa Kodi na Halmashauri za Miji/Majiji. Aidha, ni budi kuwepo na mgawanyo ulio wazi na bayana wa majukumu na madaraka ya mamlaka hizo. Katika miaka kumi iliyopita mfumo wa kukusanya kodi ya majengo katika Tanzania umekuwa ukibadilika mara kwa mara kati ya mfumo wa kugatua madaraka kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mfumo wa kukusanya kodi hiyo moja kwa moja kwa kutumia Mamlaka ya Ukusanyaji Kodi ya Serikaali Kuu.

Tamko La Umoja Wa Wadau Wa Haki Ya Kodi Tanzania (Ttjc): Ukusanyaji Wa Mapato Yatokanayo Na Rasilimali Za Ndani, Matumizi, Changamoto Na Mapendekezo

Imechapishwa na Policy Forum

TAMKO LA UMOJA WA WADAU WA HAKI YA KODI TANZANIA (TTJC)

UKUSANYAJI WA MAPATO YATOKANAYO NA RASILIMALI ZA NDANI, MATUMIZI, CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO

Serikali inalo jukumu kubwa la kuwapatia wananchi huduma bora za umma. Ili Serikali iweze kutimiza wajibu wake kwa umma inahitaji rasilimali mbalimbali, zikiwemo fedha. Kushindwa kwa serikali kukusanya mapato ya kutosha kunadhoofisha uwezo wake wa kutoa huduma bora kwa Watanzania.

Mapitio ya " Suala la Dola Bilioni Moja": Tanzania Inaendelea Kupoteza Kiasi Gani cha Fedha za Kodi?

Imechapishwa na Policy Forum

Serikali inalo jukumu kubwa la kuwahakikishia na kuwapatia watu wake huduma na bidhaa za umma. Hizi ni pamoja na afya, elimu, maji, miundombinu, ulinzi na usalama na kadhalika. Huduma na bidhaa hizi ni muhimu sana ili wananchi waweze kustawi na kuondokana na matatizo kama vile umaskini, ujinga na maradhi.Huduma na bidhaa za umma hugharimu rasilimali nyingi zikiwemo fedha. Fedha hizi ni za kutoka ndani na nje ya nchi. Fedha za ndani ni pamoja na mapato ya kikodi na yasiyo ya kikodi.

Maelezo ya Ripoti ya Mbeki Kuhusu Uhamishaji Haramu wa Fedha kutoka Barani Afrika

Imechapishwa na Policy Forum

Februari 2015 Jopo la Ngazi ya Juu Kuhusu Uhamishaji Haramu wa Fedha kutoka Barani Afrika, likiongozwa na Mwenyekiti wake Rais Thabo Mbeki, liliwasilisha ripoti yake kwa Tume ya Umoja wa Afrika/Tume ya Umoja wa Kimataifa ya Kiuchumi Barani Afrika (AUC/ECA). Ripoti ilionesha kuwa nchi za Kiafrika hupoteza kwa wastani dola bilioni 50 kwa mwaka kutokana na uhamishaji haramu wa fedha. Shughuli za kibiashara za sekta binafsi ndizo zinazochangia kwa kiwango kikubwa uhamishaji haramu wa fedha (IFFs), zikifuatiliwa na uhalifu uliopangwa, kisha shughuli za sekta ya umma.

Maswali Yetu Muhimu kwa Serikali ya Tanzania

Imechapishwa na Policy Forum

Mfumo wa Uongozi / utawala wa sasa wa Tanzania utafikia mwisho wake katika miezi michache ijayo. Hii inatoa njia kwa mfumo mpya kuchukua hatamu ikitegemewa kuwa na mikakati mipya au iliyoboreshwa kusukuma maendeleo ya kiuchumi.

Kampeni ya kupambana na utoroshwaji haramu wa rasilimali na fedha barani Afrika

Imechapishwa na Policy Forum

Tarehe 25 Juni 2015, Policy Forum ilishiriki kwenye uzinduzi wa kampeni “Stop The Bleeding” inayolenga kupambana na utoroshwaji haramu wa rasilimali na fedha barani Afrika. Kampeni hii ambayo inaongozwa na asasi za kiraia za kiafrika kwa ushirikiano na mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa, inaazimia kufanyia kazi matokeo ya utafiti na mapendekezo ya ripoti ya Thabo Mbeki ijulikanayo kama "the High Level Panel on Illicit Financial Flows from Africa" ambayo imechunguza tatizo la utoroshwaji wa fedha hizi.

Tamko kwa Umma:-Asasi za kiraia zapongeza juhudi ya serikali ya kuongeza mapato kutokana na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na kupunguza misamaha ya kodi

Imechapishwa na Policy Forum

Jumuiko la asasi za kiraia zinazoshawishi haki katika kodi Tanzania, zimeipongeza serikali kwa kuandaa rasimu ya Muswada wa Kodi ya Ongezeko la Thamani wa mwaka 2014 na Muswada wa Uendeshaji wa Kodi wa mwaka 2014 wenye madhumuni ya kuelekeza uendeshaji wa kodi ya  Ongezeko la Thamani na kuunda muundo wa kisasa na wenye ufanisi wa uendeshaji wa kodi. 

Subscribe to Tax