Skip to main content

Ripoti Fupi Ya Uchambuzi Wa Bajeti Ya Wizara Ya Nishati Na Madini Kwa Mwaka 2017/2018

Imechapishwa na Policy Forum

Sekta ya nishati inakabiliwa na changamoto mbalimbali hapa nchini ikiwemo: upungufu wa fedha za kutosha, ushiriki na uwekezaji mdogo wa sekta binafsi katika miradi mikubwa ya nishati; utegemezi mkubwa sana kwa tungamotaka kama chanzo cha nishati; gharama kubwa za tozo za uunganishaji na usambazaji wa umeme; upungufu wa wataalam na tafiti; uwepo na matumizi ya teknolojia miundombinu duni; na uwekezaji mdogo katika nishati jadidifu. Soma zaidi...

Uchambuzi Wa Utekelezaji Wa Mapato Na Matumizi Ya Mwaka 2016/2017 Na Makadirio Ya Mapato Na Matumizi Kwa Mwaka 2017/2018

Imechapishwa na Policy Forum

Kilimo, Mifugo na Uvuvi ni sekta muhimu sana kwa uchumi na maendeleo ya nchi na Watanzania
kiujumla. Sekta hizi zimeendelea kuwa chanzo kikubwa cha kipato kwa zaidi ya asilimia 65 ya
Watanzania na nguzo muhimu katika kuhakikisha usalama wa chakula, na zinachangia pato la taifa
kwa zaidi ya asilimia 29 na kwa mauzo ya nje zinachangia kwa zaidi ya asilimia 24.

Viwango vya Utawala Bora na Usimamizi wa Rasilimali Asilia (RGI) hutathmini jinsi nchi zenye utajiri wa rasilimali za Mafuta, Gesi na Madini zinavyojisimamia

Imechapishwa na Policy Forum

Sekta ya Mafuta na Gesi asilia ina alama 53 kati ya alama 100 za RGI 2017. Tofauti na sekta ya madini ambayo ni kongwe, Tanzania bado haijaanza uzalishaji mkubwa wa gesi baada ya ugunduzi wa gesi nyingi katika kina kirefucha bahari ya Hindi  ambayo hivi sasa inakadiriwa kuwa futi za ujazo trilioni 57. Hali ya kuridhisha ya Tanzania katika uwezekano wa kupata thamani ya rasilimali, kipengele kinachopima ubora wa utawala katika utoaji wa leseni, mfumo wa kodi, athari kwa jamii na ushiriki wa Serikali, hutegemea sana utaratibu wa kisheria wenye masharti mahimu kuhusu utawala na uwazi.

Mapitio ya " Suala la Dola Bilioni Moja": Tanzania Inaendelea Kupoteza Kiasi Gani cha Fedha za Kodi?

Imechapishwa na Policy Forum

Serikali inalo jukumu kubwa la kuwahakikishia na kuwapatia watu wake huduma na bidhaa za umma. Hizi ni pamoja na afya, elimu, maji, miundombinu, ulinzi na usalama na kadhalika. Huduma na bidhaa hizi ni muhimu sana ili wananchi waweze kustawi na kuondokana na matatizo kama vile umaskini, ujinga na maradhi.Huduma na bidhaa za umma hugharimu rasilimali nyingi zikiwemo fedha. Fedha hizi ni za kutoka ndani na nje ya nchi. Fedha za ndani ni pamoja na mapato ya kikodi na yasiyo ya kikodi.

Tamko la Kikundi Kazi cha Bajeti Kuhusiana na Bajeti ya Mwaka 2014/15

Imechapishwa na Policy Forum

Wakati Waziri wa Fedha  anapowasilisha  Bajeti ya Taifa  kwa mwaka wa Fedha 2014/15  Bungeni  kesho, sisi  Wajumbe wa  Kikundi Kazi cha Bajeti  cha  Policy Forum, tunaowakilisha zaidi ya Asasi  70 za Kiraia tuliounganisha nguvu zetu  ili kuongeza uelewa na  ushiriki wa jamii katika uandaaji wa sera, tunapenda kutoa  mchango wetu katika mchakato huu  muhimu.   

Tamko La Kikundi Kazi Cha Bajeti Cha Policy Forum Juu Ya Taarifa Ya Mdhibiti Na Mkaguzi Mkuu Wa Serikali (Cag) Ya Mwaka 2011/2012

Imechapishwa na Policy Forum

Juma lililopita, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) aliwasilisha Bungeni taarifa yake ya  mwaka kuhusu mahesabu ya serikali kwa mwaka ulioishia Juni 30, 2012 kufuatana na ibara ya 143  ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu cha 34 cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma Na: 11 ya mwaka 2008.  Taarifa inaonyesha baadhi ya masuala ambayo yanazuia ufanisi wa Serikali kuu, Serikali za mitaa, Mamlaka za umma na vyombo vingine kufikia malengo yao.

Subscribe to Budget issues