Skip to main content

Ileje Environmental Conservation Association (IECA)

Imechapishwa na Policy Forum

Ileje Environmental Conservation Association (IECA), ni asasi isiyo ya kiserikali inayofanya kazi katika sekta ya mazingira iliyoundwa na jamii ya wilaya ya Ileje mkoani Mbeya kwa lengo la kuwakutanisha wanakijiji katika kuhifadhi mazingira kwa maendeleo yao endelevu. Ilianzishwa mwaka 2004 chini ya Sheria ya Jamii na ikapewa Cheti No 1255. IECA inasimamia jukumu lake la kuhakikisha usimamizi endelevu wa mazingira katika maeneo yake ya mamlaka.

Lawyers’ Environmental Action Team (LEAT)

Imechapishwa na Policy Forum

Lawyers’ Environmental Action Team (LEAT) ni asasi isiyo ya kiserikali na isiyo jiendesha kwa faida inayojishughulisha na usimamizi na ulinzi wa mazingira nchini Tanzania. LEAT imejikita katika shughuli za utafiti katika usimamizi wa maliasili haswa katika ardhi, madini, wanyamapori, rasilimali za maji na misitu. LEAT inajishughulisha na kutetea marekebisho ya kisheria na sera katika utunzaji wa mazingira na usimamizi wa maliasili.

Subscribe to Environment