
Richard Angelo ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo alisoma Shahada ya Sanaa katika Sosholojia na kuhitimu mnamo 2006, Hapo awali alifanya kazi HakiElimu na baadaye kama mshauri katika kitengo cha habari. Alijiunga na Policy Forum mwaka 2008 kama Msaidizi wa Programu- Vyombo vya Habari, Mawasiliano na Uchechemuzi na kwa sasa ni Meneja wa Tawaka Serikali za Mitaa. Yeye pia ni mhitimu wa mafunzo ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji katika Utumishi wa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Rhodes, Afrika Kusini na pia amehudhuria pia Mafunzo ya Wakufunzi (ToT) ya SAM.