Judith Urio ni Mkuu wa Idara ya Vijana kutoka shirika la UNA na ni Mratibu wa Jukwaa la Maendeleo Endelevu Tanzania (TSDP), linalounganisha zaidi ya asasi 500 za kiraia ili kuendeleza utekelezaji, ufuatiliaji na utoaji wa taarifa kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs). Aliongoza uandaaji wa Taarifa ya Mapitio ya Kitaifa ya Hiari ya Asasi za Kiraia ya mwaka 2023, akihakikisha mitazamo ya wananchi wa ngazi za chini na mashirika ya kiraia inawakilishwa katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.
Akitambulika kama mtaalamu wa utekelezaji na utoaji wa taarifa za SDGs, Judith pia ni kiongozi kijana anayefanya uchechemuzi wa haki za kiuchumi na ushirikishwaji katika maamuzi. Ana Shahada ya Kwanza ya Mahusiano ya Kimataifa na Diplomasia.