TAARIFA KUHUSU HALI YA TANZANIA BAADA YA UCHAGUZI NA MASUALA YA HAKI ZA BINADAMU
Policy Forum inasikitishwa na taarifa za vifo vya wananchi, ukiukwaji wa haki za binadamu na changamoto nyingine za utawala bora zilizojitokeza katika kipindi kilichofuata baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2025. Tunaungana na Watanzania wote kuomboleza wale waliopoteza maisha na tunatoa pole kwa familia zote zilizoathirika.