Skip to main content

Mjue Diwani (Toleo la Tatu)

Imechapishwa na Policy Forum

Ndugu msomaji, tunayo furaha kukuletea kitabu kipya kiitwacho “Mjue Diwani” ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wetu wa Kikundi Kazi cha Serikali za Mitaa wa kuwaelimisha wananchi kuhusu utawala wa Serikali za Mitaa na
kukuza uwajibikaji katika jamii.

Maazimio Na Mapendekezo Ya Waheshimiwa Madiwani Baada Ya Kushiriki Mafunzo Ya Uongozi Na Uwajibikaji Wa Kijamii

Imechapishwa na Policy Forum

Sisi Waheshimiwa madiwani tulioshiriki warsha ya mafunzo ya uongozi na uwajibikaji wa kijamii iliyoandaliwa na kuratibiwa na Kinkundi kazi cha Serikali za Mitaa cha Policy Forum kwa kushirikiana na halmashauri ya Kiteto kati ya tarehe 18 hadi 23 Julai 2016,

Baada ya kupokea na kujadili mada mbalimbali, tumetambua umuhimu wa nyaraka na taarifa mbalimbali kwenye hatua zote za usimamizi wa rasilimali za umma na mfumo wa uwajibikaji jamii,

Mjue Diwani (Toleo la Pili)

Imechapishwa na Policy Forum

Ndugu msomaji, tunayo furaha kukuletea kitabu kipya kiitwacho “Mjue Diwani”  ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wetu wa kikundi kazi cha serikali za mitaa wa kuwaelimisha wananchi kuhusu utawala wa Serikali za Mitaa na kukuza uwajibikaji katika jamii. Kusoma zaidi bofya hapa

Tamko la Kikundi Kazi cha Serikali za Mitaa cha Policy Forum kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014

Imechapishwa na Policy Forum

Sisi wajumbe wa Kikundi Kazi cha Serikali za Mitaa cha Policy Forum, tunaowakilisha zaidi ya Asasi  70 za Kiraia tuliounganisha nguvu zetu  ili kuchangia katika kuifanya michakato ya sera ngazi ya serikali za mitaa kuwa yenye uwazi zaidi, ya kidemokrasia, iliyo shirikishi na yenye uwajibikaji, tunapenda kutoa  mchango wetu katika mchakato huu  muhimu wa uchaguzi wa serikali za mitaa wa 2014.  

Utawala wa Kidemokrasia katika Jamii (5th Edition, 2011)

Imechapishwa na Policy Forum

Mwananchi ana wajibu na majukumu yake kuhakikisha kuwa Kiongozi aliyemchagua au kuteuliwa anatimiza wajibu wake ipasavyo katika viwango vinavyokubalika katika eneo la kijiji/mtaa kulingana na mipango na makubaliano ya vikao vya kisheria vya kijiji na mtaa. Kila mwananchi ana wajibu wa kupinga na kukataa kila aina ya uovu katika jamii ikiwemo rushwa, uonevu, wizi, ubadhirifu wa mali za umma na ya watu binafsi. Kwa maelezo zaidi tafadhali angalia viambatanisho hapo chini.

Utawala wa Kidemokrasia katika Jamii

Imechapishwa na Policy Forum

Mwananchi ana wajibu na majukumu yake kuhakikisha kuwa Kiongozi aliyemchagua au kuteuliwa anatimiza wajibu wake ipasavyo katika viwango vinavyokubalika katika eneo la kijiji/mtaa kulingana na mipango na makubaliano ya vikao vya kisheria vya kijiji na mtaa. Kwa taarifa kamili tafadhali bofya hapa.

Utawala Wa Kidemokrasia Katika Jamii: Ushiriki Wa Wananchi Katika Serikali Za Mitaa (Vitongoji, Vijiji Na Mitaa)

Imechapishwa na Policy Forum

Kikundi Kazi cha Serikali za Mitaa cha Policy Forum (LGWG) kimechapisha tafsiri rahisi ya kanuni za utawala kijijini. Kitabu hicho kinachoitwa 'UTAWALA WA KIDEMOKRASIA KATIKA JAMII: USHIRIKI WA WANANCHI KATIKA SERIKALI ZA MITAA (VITONGOJI, VIJIJI NA MITAA)', kinalenga kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika mipango ya maendeleo katika vijiji na mitaa. Kama kawaida ya Policy Forum, kitabu hiki kiko kwa lugha rahisi na katuni ili kumpa hamu msomaji na kuongeza uelewa zaidi wa ujumbe kwa kile kilichokusudiwa kufika kwa mwananchi wa kawaida.

Subscribe to Local Governance