Uswisi kushirikiana na Tanzania kuimarisha uwajibikaji
Ubalozi wa Uswisi hapa nchini kupitia Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi SDC umezindua awamu ya tatu ya programu ya uwajibikaji wa kijamii (Social Accountability Programme - SAP) ambayo inachangia kuziwezesha asasi za kiraia (AZAKI) zinazofanya kazi ili kuboresha uwajibikaji nchini Tanzania.