Mpango wa Mwaka wa 2021 unawasilisha maeneo muhimu ya kipaumbele ambayo mtandao wa PF unakusudia kutekeleza katika mwaka wake wa kwanza wa mpango mkakati wa miaka 4 (2021-2024) na jinsi itakavyopima mafanikio ya kazi zake ili kuchangia Kuboresha maisha bora kupitia usawa katika matumizi ya rasilimali za umma na utawala shirikishi. Ili kufanikisha mabadiliko yanayotarajiwa ambayo yanasisitiza maono na dhamira ya PF, utekelezaji wa mpango huu wa kila mwaka unakusudia kuathiri michakato ya sera zinahusiana na uwajibikaji ulioimarishwa na utumiaji unaozingatia usawa wa rasilimali za umma kupitia kuimarishwa kwa ushirikiano mzuri na wa kimantiki na serikali.
Mpango huu wa kila mwaka sio tu unaonyesha kazi ambazo PF fanya katika kipindi cha 2021 lakini pia itatoa ripoti dhidi ya utendaji wake wa kila katika mkakati mpya. Kwa mwaka 2021 PF inadhamiria kukuza matumizi ya maarifa wa wanachama na AZAKi na vile vile kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na wadau mbali mbali wenye lengo la kuongeza uwajibikaji na usawa katika utumiaji wa rasilimali za umma.
Ili kusaidia PF kufikia matokeo yake yaliyopangwa, mtandao utazingatia maeneo manne yafuatayo:
- Eneo la 1: Kuimarika kwa ushawishi wa wanachama wa PF kuhusu matumizi ya rasilimali za umma yanayozingatia usawa na uongozi shirikishi kupitia maarifa na mabadiliko
- Eneo la 2: Kuimarika kwa ushirikishaji unaozingatia maamuzi ya pamoja unaoboresha matumizi ya rasilimali yanayozingatia usawa na uwajibikaji
- Eneo la 3: kuendeleza ujifunzaji shirikishi utakaozingatia mabadilio na kuchagiza ubia ambao utafanya uchechemuzi wenye shuhuda ili kuimarisha uongozi shirikishi
- Eneo la 4: Uborekaji wa kitaasisi yenye uwezo wa kusimamia rasilimali zake