Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/2017-2020/21), pamoja na malengo mengine, unakusudia kuweka mazingira wezeshi kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kujiajiri na kushiriki katika shughuli za kiuchumi kama vile kilimo, ufugaji na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.
Miongoni mwa mikakati ya kutimiza lengo hilo iliyoainishwa katika Mpango huo ni utoaji wa mikopo yenye gharama na masharti nafuu kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.
Katika kutekeleaza Mkakati huo, Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa, Sura ya 290 ilifanyiwa marekebisho mwaka 2018 ili kuweka masharti kwa Halmashauri zote nchini kutenga fedha kwa ajili ya mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. Kufuatia marekebisho hayo, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ilitunga kanuni zinazoainisha masharti ya utoaji wa usimamizi wa mikopo inayotolewa na Halmashauri kwa vikundi hivyo. Kusoma zaidi kuhusiana na masharti na kanuni za utoaji na usimamizi wa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu bofya hapa