Skip to main content
Picha ya vipeperushi tayari kwa kupelekwa kwa wananchi

Mradi Wa Elimu Ya Mpiga Kura Halmashauri Ya Wilaya Ya Muheza August — October 2020

Na Alex Mbwilo

Mradi wa elimu ya mpiga kura katika halmashauri ya Muheza ulilenga kuongeza uelewa wa jamii juu ya umuhimu wa kushiriki katika shughuli za kisiasa kwa kuhudhuria mikutano ya kampeni ili kujua sera za vyama vya siasa na wagombea wa  uongozi ngazi ya udiwani, ubunge na Raisi na kwa hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya  kuchagua wagombea  hao  kutokana na sera zao na vyama katika kuliongoza Taifa katika kipindi cha miaka mitano. Aidha  elimu hiyo ililenga pia katika kuhamasisha wananchi wajitokeze siku na tarehe iliyopangwa kwa ajili ya kupiga kura.

Mradi ulilenga kutekelezwa katika kata 37 ambazo zipo katika halmashauri ya wilaya ya Muheza, Hata hivyo kutokana na changamoto ya rasilimali fedha mradi ulitekelezwa katika kata 21. Pamoja na hivyo ililazimika kupunguza baadhi ya mbinu za utekelezaji kutoka mbinu zilizoandaliwa wakati wa kubuni na kuutayarisha mradi wenyewe.

Matokeo tarajiwa ya mradi

Ilitarajiwa baada ya utekelezaji wa mradi mambo yafuatayo yatatokea:-

  1. Mahudhurio ya wananchi katika mikutano ya kampeni inayofanywa na wagombea kutoka vyama vya siasa yataongezeka.
  2. Watu wengi wameshiriki zoezi la kuchagua viongozi wao siku ya tarehe 28/10/2020.

Ili kuthibitisha mafanikio ya mradi basi dalili zifuatazo zitaonekana:

  1. Idadi ya wananchi vyanaojitokeza kuhudhuria katika mikutano ya kampeni ya  wagombea na vyama vya siasa.
  2. Idadı ya wananchi waliojitokeza siku ya kııpigakura
  3. Kiasi cha kura zilizoharibika wakati wa uchaguzi

Wakati wa utekelezaji wa mradi huu ambao umetekelezwa katika kata  21 ambazo ni Majengo, Genge, Mbaramo, Tanganyika, Masuguru, Kwemkabala, Kilulu, Tingeni, Bwembwera, Ngomeni, Lusanga, Songa, Kwafungo, Kwebada, Amani, Mhomole, Misalai, Kicheba, Misozwe, Nkumba na Tongwe, kulifanyika  kazi kadhaa kama ifuatavyo.

  1. Kununua T-shirts 150 na kuzichapisha ujumbe kuhusu uchaguzi kama ulivyo na kiliwa kutoka Tume ya uchaguzi na kuzigawa kwa jamii
  2. Kopi 10,000 za kipeperushi cha Tume ya uchaguzi kuhusu uchaguzi na kukigawa kwa watu mbalimbali katika mikusanyiko na majumbani lakini pia katika shule za sekondari
  3. Kutoa elimu ya mpiga kura kupitia mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali.
  4. Kutoa elimu ya mpiga kura kwa kuwapitia walengwa katika masoko, vijiwe vya  bodaboda, standi za magari na mitaa ya makazi ya watu.
  5. Kujadiliana na wapiga kura kwa kuulizana maswali kuhusu uchaguzi na kupeana majibu juu ya maswali hayo.

Baada ya kazi ya kutoa elimu ya mpiga kura kukamilika tarehe 27/10/2020 uongozi wa Sakale Development Foundation ulitoa maelekezo kwa wafanyakazi wa mradi kuamka mapema na kuwahi kufika katika vituo vyao walivyojiandikisha kupiga kura na wapige kura wakiwa wa kwanza au wasizidi watatu katika kituo cha kupiga kura ili baada ya hapo wawe  wanapita  katika  maeneo  mbalimbali  na  hasa  ya  vijiwe  kuona  kama  wananchi

wanaelekea  katika  vituo  vya kupiga  kura na wanapiga  kura.  Siku  ya tukio,  wafanyakazi  wa mra‹ii walitekeleza maelekezo hayo na kwa walibaini yafuatayo:-

  1. Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa kwa wakati
  2. Wananchi wengi walielekea katika vituo vya  kupiga kura na walipiga kura, namba  kubwa ilikuwa ni wanawake
  3. Vijana wengi wa vijiwe na biashara va bodaboda hawakushiriki ipasavyo katika zoezi la kupiga kura.

Changamoto

Wakati wa utekelezaji wa mradi huu asasi na watendaji wake wameI‹utana na changamoto mbalimbali:-

  1. Ufinyu wa bajeti kwa ajili ya kazi za mradi na kwa hiyo kushindwa kutekeleza mradi katika kata zote 37 kama ilivyo pangwa awali.
  2. Baadhi ya washiriki waliohusika katika  vikao au mijadala juu ya elimu ya mpiga kura walikuwa wanaomba malipo ya ushiriki wao.

Mambo tuliyojifunza

Tumejifunza elimu ya mpiga kura ni suala muhimu sana kwa wananchi wengi kwa kuwa tulikuwa tunaulizwa maswali ambayo ungetegemea wapiga kura ›valikuwa wanayajua kabla ya kazi hii kwa kuwa ni shughuli ambayo imekuwa ikifanyika kila mwaka wa uchaguzi.

Mfano:-mtu hajui muda wa kufunguliwa na kufungwa vituo vya kupigia.

Mtu kwakuwa hajahakiki taarifa zake wakati wa mazoezi hayo na hajahama eneo la makazi hajui kama anastahili kupiga kura, ana amini kwa kuwa  hakuhakiki kwahiyo amekosa sifa ya kupiga kura!.

Mapendekezo

Sakale Development Foundation ikiwa ’asasi ambayo imetekeleza mradi huu ina maoni na mapendekezo kadhaa kwaTume ya taifa ya Uchaguzi kama ifuatavyo:

Kazi ya kutoa elimu ya mpiga kura ni jambo muhimu na lenye kuhitajika sana. Linahitaji muda wa kutosha na rasimali za kutosha. Asasi nyingi zilizopewa vibali hwa ajili ya kazi hii hazikuwa na fedha na kwa hiyo zimepata shida sana katika kufikia malengo waliyojiwekea. Tunashauri vibali vya kutoa elimu ya mpiga kura katika siku na miaka ijayo vitolewe mapema iwezekanavyo ili asasi zitakazo kuwa zimepata vibali hivyo ziweze kuvitumia katika kutafuta fedha kwa wadau wa mbalimbali wa maendeleo.

Makala hii imeandaliwa na Alex Mbwilo, Katibu Mtenadaji wa Sakale Development Fundation (SADEF)