Skip to main content
Imechapishwa na Policy Forum

Guluka Youth Environment Group (GYEG) ni asasi isiyo ya kiserikali ambalo lilianzishwa mnamo tarehe 22 Septemba, 2003 na kikundi cha vijana wakiwa na mpango wa kutaka kuwezesha jamii za pembezoni hasa vijana katika maeneo ya uhifadhi wa mazingira, utawala bora na haki za binadamu na jinsi ya kukabiliana na  VVU/UKIMWI na matumizi ya dawa za kulevya.

Asasi hii inafanya kazi zifuatazo:

 a. Kuongeza uwazi na uwajibikaji ili kuimarisha utawala bora, haki za binadamu, uhifadhi wa mazingira na kuongoza mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya na jinsi ya kukabiliana na VVU/UKIMWI katika jamii.

b. Kuanzisha na Kuendeleza mipango mbalimbali inayohusu mazingira na kutumia rasilimali za umma kama vile misitu, ardhi, maji na wanyamapori.

c. Kuendesha programu juu ya Utawala Bora, Haki za Binadamu na usawa wa kijinsia ili kuimarisha uwazi na uwajibikaji kwa viongozi wa serikali na jamii kwa ujumla.

d. Kuandaa programu ambazo zitakuza uchumi na mawasiliano kama zana za maendeleo ya jamii.

 e. Kuanzisha programu ambazo zitachochea matumizi sahihi ya rasilimali za umma ili ziweze kukidhi mahitaji ya vizazi vya sasa na vijavyo.

 g. Kuendeleza programu za kuwezesha wanawake, vijana na vikundi vingine ndani ya jamii kwa malengo ya kupunguza umaskini.

-6.8049460165601, 39.262868878483