Kuibuka kwa ukatili wa hivi karibuni nchini Afrika Kusini ni suala la kutia huzuni kubwa kwa nchi hiyo, kanda yote ya SADC na bara la Afrika kwa ujumla. Kwa bahati mbaya mashambulizi haya mapya yaliyolengwa dhidi ya watu wanaotazamwa kama “wageni” sio matukio ya nadra yanayofanywa na wahalifu wachache. Sasa ni wazi bila kupinga kuwa hali ya kibaguzi dhidi ya waafrika wenzao imeongezeka miongoni mwa raia nchini Afrika Kusini, jambo ambalo linakinzana na Sera za SADC zinazohimiza umoja, ushirikiano, usalama na uhuru wa raia kusafiri na kufanya shughuli za kiuchumi katika nchi wanchama ili mradi wanazingatia sheria na taratibu zilizokubalika ndani ya SADC. Soma zaidi (PDF):