Wafanyakazi Wetu

Richard Angelo    | Meneja-Serikali za Mitaa

 

 

 

 

 

 

 

Richard Angelo ni muhitimu wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo alimaliza shahada yake ya Sanaa na Jamii mwaka 2006, Kabla ya kujiunga Policy Forum alifanya kazi shirika la HakiElimu kama mkufunzi na mshauri katika kitengo cha mawasiliano. Alijiunga na Policy Forum mwaka 2008 kama Msaidizi wa Programu-Habari, Mawasiliano na Uchechemuaji na sasa hivi ni Meneja wa Serikali za Mitaa. Anapendelea kuandika na mambo ya maendeleo ya jamii.

Nicholas Lekule  | Meneja-Sera na Uchambuzi wa Bajeti

 

 

 

 

 

 

 

Nicholas Lekule alijiunga na Policy Forum Mei 2013 katika nafasi ya Meneja wa  Uchambuzi wa Sera na Bajeti. Kabla ya kujiunga na Policy Forum, awali alifanya kazi katika shirika la Sikika kama Afisa wa Programu, nafasi ambayo aliishika kwa miaka mitano. Uzoefu wake ni katika eneo la uchambuzi wa bajeti na utawala kwa ujumla. Nicholas ana Shahada ya Sanaa katika Sosholojia aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2007. Pia alihudhuria kozi kadhaa za muda mfupi ndani na nje ya nchi ili kuweza kuboresha ujuzi wake. Anapendelea kuona sera zetu zinafanya kazi kwa ajili ya watanzania wengi.

      Semkae Kilonzo | Mratibu
 
 
 
 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Semkae Kilonzo alianza kazi Policy Forum mwaka 2007 kama Meneja anayehusika na habari, Mawasiliano na Uchechemuaji katika ofisi za mtandao wa sekretarieti, Sehemu ya matamanio yake ni kuona taarifa za uchambuzi wa sera zina sambazwa ipasavyo kwa watengeneza sera, asasi za kiraia na raia wote kwa ujumla. Na kwa sasa ni Mratibu, anayeongoza sekretarieti. Semkae ana shahada ya uzamili katika uandishi wa habari na masomo ya habari katita chuo cha Cardiff, Uingereza na kupata mafunzo ya habari Dublin Ireland na Shule ya Uandishi wa Habari Tanzania, Anapendelea kuhimiza watu wote kujihusisha katika shughuli za kutengeneza sera.                     

      Rashid Kulewa | Dereva

 
 

 

 

 

 

 

 

Rashid Kulewa alijiunga sekretarieti ya Policy Forum mwaka 2010, Alimaliza kozi yake ya kompyuta ICL Training Centre na amefanya kazi na mashirika tofauti kama FHI amabapo alikuwa kama dereva na Axios Foundation kama dereva na msaidizi wa afisa mgavi. Rashid anapendelea kuona watu wa Tanzania wanafaidika na mali asili za nchi yao.

Gibons Mwabukusi | Meneja wa Utawala na Fedha

Gibons Mwabukusi alijiunga Policy Forum mwaka 2010 kama Afisa Utawala na Fedha.Kabla ya kujiunga na Policy Forum alifanya kazi na mashirika tofauti yasiyo ya kiserikali katika mambo ya utawala na fedha. Ana stashahada ya juu ya uhasibu aliyopata kutoka Taasisi ya Uhasibu Tanzania. Matamanio yake ni kuona Policy Forum ikiwa mbele katika kuhamasisha utawala bora na uwajibikaji.

Amani Ndoyella | Msaidizi Utawala

 
 

 

 

 

 

 

 

Amani Ndoyella alijiunga na Sekretarieti ya Policy Forum mwaka 2004 baada ya kumaliza masomo yake ya National Board for Materials Management (NBMM). Na sasa hivi anahusika na utaratibu wa ugavi,orodha/hesabu za ofisi na kukatalogi taarifa muhimu kwa wanachama wa Policy Forum. Amani anapendelea kuona mali asili za Tanzania zinatumika ipasavyo ili kuleta maisha bora kwa watu wote wa Tanzania.

Iman Hatibu
 Afisa Programu Msaidizi- Uchechemuzi na Ushirikishaji
 

Iman Hatibu alijiunga na Policy Forum 2017 kama Msaidizi wa Programu-Uchechemuzi na Ushirikishaji. Iman ana elimu ya sheria ambayo aliipata Chuo Kikuu cha Tumaini. Kabla ya kujiunga na Policy Forum alikuwa akifanya kazi UN Association of Tanzania kama msimamizi wa programu. Amefanya kazi katika tasnia ya Mawasiliano na Utetezi wa Maendeleo Endelevu, Haki za Binadamu, Utawala Bora, Demokrasia, Amani na Usalama. Iman ana uzoefu katika kutetea masuala mbalimbali ya haki za binadamu, baada ya kushiriki katika harakati za haki za binadamu tangu umri mdogo. Ana uwezo wa kipekee wa kuelewa ugumu wa haki za binadamu na masuala ya kijinsia

Prisca Kowa
Afisa Programu Mwandimizi-Serikali za Mitaa na Uhusiano na Wadau
 

Prisca Kowa ni muhitimu wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo alipata shahada yake ya Elimu ya Jamii, 2009. Kwa sasa anamalizia masomo yake ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Prisca alijiunga na Policy Forum kama Msaidizi wa Programu-Uwezo na Uwezeshaji 2011 kisha 2018 aliongezewa majukumu na kuwa Afisa Programu Mwandamizi Serikali za Mitaa na Uhusinao na Wadau. Amefanya kazi na CARE International na Aga Khan Foundation, akijihusisha na mambo ya jamii. Prisca anapendelea kujihusisha na mambo ya uchambuzi wa sera na kazi za jamii kwa ujumla.

Hellen Massawe | Afisa Programu Msaidizi-Sera na Uchambuzi wa Bajeti

 

Hellen Massawe alijiunga na Policy Forum 2017 kama Afisa Programu Msaidizi- Uchambuzi wa Bajeti na Sera. Ni mhitimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alipata shahada ya Sheria. Baada ya kupata shahada ya sheria alijiunga na Shule ya Sheria Tanzania na kuhitimu mwaka 2017. Hellen hupendelea kujishughulisha na mambo ya kimaendeleo.

Amne Islam | Afisa Programu-Ufuatiliaji na Tathmini (MEL)

Amne Hamid alijiunga na Policy Forum kama Afisa wa Ufuatiliaji na Tathmini (MEL). Amne ana jukumu la kuongoza shughuli za MEL ndani ya shirika. Amne ana uzoefu wa zaidi ya miaka 3 katika tasnia wa MEL na ana shahada ya Maendeleo ya Jamii kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa. Ana uzoefu wa kubuni mifumo na mipango ya MEL kuandaa zana za kukusanya taarifa, kuhakikisha ubora wa taarifa, kufanya uhakiki wa miradi na kufundisha watumiaji wa mfumo wa MEL. Ana uzoefu wa kufuatilia miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na ya elimu ya vijana, jinsia na afya za uzazi na ujasiriamali. Amepata ujuzi huo baada ya kufanya kazi na wafadhili kama vile SIDA, UNICEF, DFID, Novo na Global Fund. Pia amefanya kazi na Restless Development and Population Services International (PSI). Amne anatamani kuona MEL ikifanya kazi kwa ufanisi ndani ya Policy Forum.

Elinami John | Meneja-Uchechemuzi na Ushirikishaji

Elinami John alijiunga na Policy Forum, 2016. Kabla ya hapo alikuwa Afisa Programu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT). Alikamilisha shahada yake ya kwanza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania. Ana shahada ya Uzamili katika masomo ya mawasiliano na habari kutoka Chuo Kikuu cha Karlstad, Sweden. Anapendelea kuchunguza mienendo na maendeleo ya utandawazi wa vyombo vya habari na mawasiliano na athari zake kwa jamii. Anatamani kuona Serikali ikitumia rasilimali kwa kuzingatia mahitaji na vipaumbele vya wananchi.

 
 
Swahili

Marejeo ya Mkukuta

Social Media

We are on Facebook!


drupal hit counter