Madhumuni

Policy Forum ni mtandao wa asasi zisizo za kiserikali. Mtandao huu unaokua kwa kasi, hivi sasa una asasi wanachama zaidi ya sabini ambazo zote zimesajiliwa hapa Tanzania. Nia ya Policy Forum ni kufanya sera zinufaishe watanzania kwa ujumla, na hasa zaidi watu walio katika hali ya umaskini.

Kama mtandao unaoendeshwa na asasi wanachama, Policy Forum inatazamia kuwezesha jamii kwa ujumla kujihusisha katika michakato ya uundwaji na utekelezaji wa sera huku ikilenga zaidi uondoaji wa umaskini, usawa, na ukuzwaji wa demokrasia nchini. Shughuli za Policy Forum hasa zimelenga katika sehemu tatu: utawala katika serikali za mitaa, matumizi ya fedha za umma, na ukuzaji wa sauti ya umma katika sera na mikakati mbalimbali kwa kupitia wanachama wake.

Ikishirikiana na asasi na taasisi zingine, Policy Forum inaendesha shughuli zake kwa kuhamasisha na kutetea sera zilizoboreshwa kwa njia ya uchambuzi madhubuti. Siku za nyuma, Policy Forum imewahi kuhusika katika programu ya Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Tanzania (MKUKUTA), tathmini ya matumizi ya pesa za umma, na mikutano ya umma katika uundwaji wa sheria. Policy Forum hutoa habari mbalimbali kuhusiana na michakato ya uundwaji wa sera, uchambuzi, takwimu, na tafiti kupitia vyombo vya habari kama redio, runinga, magazeti, machapisho na tovuti.

Swahili

Marejeo ya Mkukuta

Social Media

We are on Facebook!


drupal hit counter