Policy Forum ni asasi huru yenye malengo ya kuhusisha wananchi, asasi zisizo za kiserikali, na sekta zote zingine za jamii katika michakato ya uundwaji wa sera. Dhamira hii pia inahusisha kuwezesha hatua zote za michakato ya uundwaji wa sera zinaelimisha wananchi, zinakuza uwezo wao wa kujihusisha na zinaendeshwa kwa njia inayotoa nafasi ya uwajibikaji.Dira: Kuboresha maisha ya wananchi wa...

Utawala wa Kidemokrasia Katika Jamii (Toleo la 8)

UTANGULIZI
Mwananchi ana wajibu na majukumu yake kuhakikisha kuwa Kiongozi aliyemchagua au kuteuliwa anatimiza wajibu wake ipasavyo katika viwango vinavyokubalika katika eneo la kijiji/mtaa kulingana na mipango na makubaliano ya vikao vya kisheria vya kijiji na mtaa. Kila mwananchi ana wajibu wa kupinga na kukataa kila aina ya uovu katika jamii ikiwemo rushwa, uonevu, wizi, ubadhirifu wa mali za umma na ya watu binafsi.

MISWADA KUHUSU TASNIA YA UZIDUAJI: MSIMAMO WA KIKUNDI KAZI CHA AZAKI ZINAZOSHIRIKI KWENYE TASNIA YA UZIDUAJI

Categoriest

Tarehe 16 Juni 2015 Serikali ya Tanzania  ilipeleka miswada mitatu bungeni inayohusu sekta ya uziduaji chini ya “Hati ya Dharura.”  Miswada hiyo ni Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji Katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia ya mwaka 2015 (The Tanzania Extractive Industries (Transparency and Accountability) Act 2015, Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi ya mwaka 2015. (The Oil and Gas Revenue Management Act 2015)  Sheria ya Petroli ya mwaka 2015 (The Petroleum Act 2015).

Pages