Policy Forum ni asasi huru yenye malengo ya kuhusisha wananchi, asasi zisizo za kiserikali, na sekta zote zingine za jamii katika michakato ya uundwaji wa sera. Dhamira hii pia inahusisha kuwezesha hatua zote za michakato ya uundwaji wa sera zinaelimisha wananchi, zinakuza uwezo wao wa kujihusisha na zinaendeshwa kwa njia inayotoa nafasi ya uwajibikaji.Dira: Kuboresha maisha ya wananchi wa...

Tamko Rasmi:Bajeti 2016/2017

Leo Bunge la Tanzania hivi karibuni litaanza kujadili  Bajeti ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016/17 na hii itakuwa mara ya kwanza kwa bunge kukutana chini ya utawala wa  Raisi John Magufuli.  Itakuwa pia mwaka wa kwanza wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano   (FYDP II) 2016/17 – 2020/21.  Kama  mwaka wa msingi, sisi  wajumbe wa  Kikundi Kazi cha Bajeti cha Policy Forum  tunapenda tutoe mchango wetu katika mchakato huu muhimu  kwa kushirikisha maoni yetu kuhusu bajeti  iliyopita na matarajio yetu kuhusu bajeti ijayo.

Mtazamo wa Azaki Kuhusu Siku 100 za Magufuli Madarakani

Categoriest

Kabla ya uchaguzi mkuu  wa Oktoba 25, 2015, Asasi Za Kiraia (AZAKI) chini ya Kikundi Kazi  cha Bajeti cha  Policy Forum ziliandaa na kuwasilisha kijarida kinachoitwa“Vipaumbele  Vyetu Vikuu  kwa Serikali Ijayo”  kwa  vyama mbalimbali vya siasa  vilivyokuwa vinashiriki katika uchaguzi ili kutilia mkazo yaliyomo kwenye kijitabu hicho.  Kijarida hicho kilikuwa na masuala nyeti yaliyohitaji serikali ya awamu ya tano kuzingatia.  

Mjue Diwani (Toleo la Pili)

Ndugu msomaji, tunayo furaha kukuletea kitabu kipya kiitwacho “Mjue Diwani”  ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wetu wa kikundi kazi cha serikali za mitaa wa kuwaelimisha wananchi kuhusu utawala wa Serikali za Mitaa na
kukuza uwajibikaji katika jamii. Kusoma zaidi bofya hapa

Pages