Skip to main content
Submitted by Web Master on 24 August 2017

Serikali inalo jukumu kubwa la kuwahakikishia na kuwapatia watu wake huduma na bidhaa za umma. Hizi ni pamoja na afya, elimu, maji, miundombinu, ulinzi na usalama na kadhalika. Huduma na bidhaa hizi ni muhimu sana ili wananchi waweze kustawi na kuondokana na matatizo kama vile umaskini, ujinga na maradhi.Huduma na bidhaa za umma hugharimu rasilimali nyingi zikiwemo fedha. Fedha hizi ni za kutoka ndani na nje ya nchi. Fedha za ndani ni pamoja na mapato ya kikodi na yasiyo ya kikodi. Upatikanaji wa mapato ya kutosha na hasa kwa njia ya ulipaji, utunzaji na utumiaji mzuri wa fedha zote na hasa zitokanazo na kodi ni jambo lisiloepukika.

Mnamo mwaka 2012, viongozi wa dini kutoka Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Baraza chini ya Kamati ya Viongozi wa dini ya masuala ya Haki za Kiuchumi na Uadilifu katika Uumbaji (Interfaith Standing Committee on Economic Justice and Intergrity of Creation-ISCEJIC). ikiwa ni pamoja na kupitia misamaha ya kodi, utoroshwaji fedha kwenda nje ya nchi na kadhalika.

Soma zaidi ...